Loading...
title : WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO
link : WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO
WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO
Na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii,Mkuranga
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imepiga marufuku wakazi wa Wilaya hiyo na wanafunzi kutovuka katika mito,na badala yake watumie njia za barabara ili kuepuka kuzama katika maji ikiwamo kuumizwa na wanyama katika mito hiyo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Filbeto Sanga,katika kikao cha robo mwaka cha Baraza la madiwani wilayani hapo."Kutokana na mvua kunyesha katika kipindi cha mwezi wa nne na mwezi huu,miundombinu imeharibika na watu wamekuwa wakitumia mito kuvuka kwenda Shule na wengine kwenda kutafuta mahitaji.
" Sasa naomba wanafunzi na wananchi,wasitumie mito kuvuka kwani kuna baadhi ya watu walipoteza maisha pia kuna wanyama wakati katika mito hiyo," amesema.Amesema wanafunzi watano walipoteza maisha katika mvua na kuna watu makubwa ambao wamepoteza maisha,lakini wanawafuatilia ili baraza lijalo idadi yake itajulikana na kuambiwa walipoteza maisha.
Amesema kutokana na mvua kunyesha miundombinu imeharibika na baadhi ya kaya nyumbani zao zimejaa maji na hari hiyo ilisababisha kuyahama makazi.Wakati huo huo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Juma Abeid amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kupata hati safi kutokana na kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ambayo imekamilika kwa wakati.
Akizungumza katika baraza la madiwani alisema kuwa,Serikali kila mwaka wanafanya ukaguzi katika halmashauri zote nchini na kama halmashauri itakuwa haikufanya vizuri inapata hati chafu.Amesema kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wakuu wa idara na madiwani,wameweza kufanya kazi kwa pamoja na kufanikisha fedha za miradi ya maendeleo kutumika kama ilivyokusudiwa,kukaa vikao kwa wakati na kusimamia fedha vizuri za halmashauri.
"Yote hayo tumeyafanya kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani na tukafanikiwa kupata hati safi," amesema Juma Abeid.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Dk Stephen Mwandambo (wapili kutoka kushoto) akiwa na watendaji wa wilaya hiyo katika mkutano wa robo mwaka wa baraza la Madiwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbeto Sanga akizungumza Michuzi juu ya kupiga marufuku kwa wananchi na wanafunzi kutokuvuka mito badala yake watumie njia za barabara ili kuepuka kuzama katika maji na kuumizwa na wanyama katika mito hiyo (kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza katika mkutano wa robo mwaka wa baraza la madiwani.
Hivyo makala WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO
yaani makala yote WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/wakazi-mkuranga-wapigwa-marufuku-kuvuka.html
0 Response to "WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO"
Post a Comment