Loading...
title : WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA
link : WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA
WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA
JUMLA ya watu 129 wanaodhaniwa Kuwa ni wahamiaji wasio rasmi wamekamatwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wakiwa wamejitokeza katika mchakato wa uandikishwaji wa Vitambulisho vya taifa .
Akizungumza jana baada ya kutembelea Kituo cha Murusi wilayani humo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema watu hao ambao si raia wa Watanzania wamebainika wakiwa wamefika katika vituo vya kujiandikishia ili wapate vitambulisho hivyo jambo ambalo si halali kwa mtu ambaye si raia kuingia kwenye mchakato huo.
Brigedia Gaguti amesisitiza hawata mvumilia yeyote atakaeingilia mchakato huo wakati akitambua yeye si raia na amewataka Wasimamizi kuhakikisha sheria na tararibu zinafuatwa na kuwabaini wote ambao si raia.
"Tumewashikilia watu hao kutokana na ushirikiano wa wananchi na maofisa wa uhamiaji.Endapo tutabaini raia wa Burundi au Congo kaingilia mchakato huu hatuta sita kumchukulia hatua, niwaombe wale wote ambao si raia mjitokeze kabla hatujaanza kuwabaini,"amesema
Brigedia Gaguti.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amekuwa mstari wa mbele kufuatilia mchakato huo mkoani Kigoma na kuwasisitiza wananchi Mkoani kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo watabaini kuna mtu ambae si raia anaingilia mchakato huo kwani endapo watapata vitambulisho watavitumia vibaya kuichafua Nchi ya Tanzania.
Amesema atahakikisha anashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha zoezi hilo linaenda sawa sawa na kusimamia zoezi hilo ipasavyo na kwa weredi mkubwa kutokana na muingiliano uliopo katika mkoa huo.
Hivyo makala WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA
yaani makala yote WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/watu-129-ambao-si-raia-wa-tanzania.html
0 Response to "WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA"
Post a Comment