Loading...
title : WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN
link : WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN
WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN
Na Said Mwishehe,Blogu ya jamiii
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya Afrika Mashariki ya kuhifadhi Koraan yanayotarajia kufanyika Uwanja wa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakati anazungumzia uwepo wa mashindano manne ya kuhifadhi Koraan ambayo yatafanyika kwa nyakati tofauti katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sheikh Alhad amefafanua katika kipindi hiki cha Ramadhan katika Mkoa wa Dar es Salaam kutakuwa na mashindano manne ya kuhifadhi Koraan na kueleza Mei 20 mwaka huu yatafanyika mashindano ya kuhifadhi Koraan kwa Afrika Mashariki na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Majaliwa.
Mbali ya Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi pia anatarajiwa kuwepo Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu Mohammed Ghalib Bilal pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Al-Manahilul Islamic Centre.
Pia Mei 26 mwaka huu yatafanyika mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Koraan yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Suluhu Foundation yanayotarajia kufanyika Mnazi Mmoja jijini.Mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk.Hussein Mwinyi pamoja na viongozi wengine kadhaa.
Sheikh Alhad ameongeza Mei 27 mwaka huu yatafanyika mashindano yatakayohusisha Bara zima la Afrika na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Alhakim Foundation wakati Juni 3 mwaka huu yatafanyika mashindano mengine ya kimataifa yaliyoandaliwa na taasisi hiyo na mgeni rasmi bado haijafahamika atakuwa nani.
Amefafanua mashindano hayo yanafanyika mwezi wa Ramadhan ni kutokana na ubora wa mwezi huo kwani ndio Koraan Tukufu iliteremshwa na kufafanua kijana wa Kiislamu anayehifadhi Koraan husaidia kuishi kwenye misingi ya maadili mema kwani atakuwa anajua nzuri na baya.
Hivyo makala WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN
yaani makala yote WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/waziri-mkuu-anatarajiwa-mgeni-rasmi.html
0 Response to "WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN"
Post a Comment