Loading...
title : ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE
link : ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE
ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE
Na Anthony Ishengoma WAMJW
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa kati ya asilimia 7 na 16 ya wanawake wote duniani ni Wajane.
Jamii imetakiwa kuendeleza mipango na kuongeza juhudi zaidi katika kukabiliana na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwainua wajane ili wapate uwezo wa kiuchumi wa kuzihudumia familia na wategemezi wao kwa kuwa ndiyo muhimili pekee wa familia iliyoachwa.
Akiongea kwa niaba ya Mgeni rasmi wa kongamano la Wajane liliofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa Bi. Honoratha Rwegasira amepongeza juhudi za wadau wa maendeleo na serikali katika kuwasaidia wajane kuleta usawa wa kinjisia na kuinua ushiriki wao katika ngazi za kutoa maamuzi.
Aidha Bi.Rwegasira ameitaka jamii kuacha mila potofu kama vile kunyanganya mali mjane, kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo, kurithi wajane na nyingine zote zinazoweza kumdhoofisha mwanamke katika jitihada zake za kujikwamua kifikra, kiutamaduni, kiuchumi,kijamii na kisiasa.
Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya,Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza amesema kimsingi lengo la maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani ni kutoa nafasi kwa Wadau kushirikiana na Serikali kwa kutoa huduma za msingi kwa wajane na kuondoa aina zote za ukandamizaji ikiwemo haki ya kumiliki mali, umasikini, mira na desturi za kurithiwa baada ya kufiwa.
Mkurugezi Msaidizi Idara ya Jinsia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza akitoa hutuba yake kwenye Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
Afisa Mwandamizi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi .Sirivia Siliwa akitoa mada kuhusu Chimbuko la Siku ya Wajane Duniani wakati wa Kongomano la Wajane lilifanyika leo Mjini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bi. Honoratha Rwegasira akitoa hutuba ufunguzi kwa niahaba ya Mgeni rasmi wakati wa Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
Wajane wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE
yaani makala yote ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/asilimia-7-hadi-16-ya-wanawake-wote.html
0 Response to "ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE"
Post a Comment