Loading...
title : Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko
link : Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko
Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kuwapunguzia gharama za ujenzi wa Mtaro wa Maji ya Mvua Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko waliojitolea kuanzisha Mradi huo kwa lengo la kujiepusha na Mafuriko yanayosababishwa na mkusanyiko wa maji mengi yanayoleta maafa wakati wa mvua za Masika.
Kauli hiyo imetolewa na Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Wananchi wa Bubujiko mara baada ya ziara fupi ya kukagua hatua za ujenzi wa Mtaro huo uliosimamiwa na Wananchi wenyewe na kuungwa mkono na Uongozi wa Mkoa na Wilaya pamoja na washirika wa maendeleo.
Balozi Seif Ali Iddi alisema kitendo cha Wananchi wa Bubujiko kujenga Mtaro huo kimekuja mara baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein kutoa kauli ya Serikali ya ujenzi wa Mtaro huo ambacho kinapaswa kupongezwa.
Alisema Serikali Kuu itaangalia namna ya kusaidia hatua iliyobaki ya kukamilika kwa ujenzi wa Mtaro huo uliobakia Mita 65 zinazotarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Milioni 30,000,000/- ambapo hadi kukamilika kwake unatarajiwa kufikia Milioni 50,000,000/-.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Umoja na Mshikamano waliyouonyesha Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko ndio chanzo cha mafanikio hayo yanayopaswa kuigwa na Wananchi wa Vijiji vyengine hapa Nchini.
“ Nafarajika kuona Mtaa wa Bubujiko kwa sasa utabakia katika Historia ya kuepuka na Mafuriko yaliyokuwa yakileta simanzi na hasara kubwa kwa Wakaazi wake”. Alisema Balozi Seif.
Mhandisiwa Ujenzi wa Mtaro wa Kijiji cha Bubujiko Bwana Bwana Mohamed Abdullah kutoka Wizara ya Kilimo, Mali Asili, Uvuvi na Mifugo Pemba akimuonyesha Ramani ya Mtaro huo Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa mbele ya Karo inayoingiza maji hayo.
Balozi Seif akiwapongeza Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko kwa hatua waliyochukuwa ya ujenzi wa Mtaro utakaonusuru na majanga ya mafuriko ya mavua.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Bubujiko wakisikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao kwenye Mtaa wa Kijiji hicho kiliopo pembezoni mwa Mji wa Wete.
Mkaazi Muathirika nambari moja wa majanga yaliyokuwa yakitokea kwenye Kijiji hicho wakati wa Mvua za Masika Maalim Omar Hamad kwa niaba ya Wananchi wenzake akiishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada inazochukuwa za kuwahudumia Wananchi wake.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko
yaani makala yote Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/balozi-seif-afanya-ziara-kijiji-cha.html
0 Response to "Balozi Seif afanya ziara kijiji cha Bubujiko"
Post a Comment