Loading...

NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA

Loading...
NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA
link : NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA

soma pia


NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lina jukumu kubwa la kuhakikisha sekta hiyo inakua na kuwafikia watu wa kipato cha chini.
Amesema ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inahimiza uchumi wa viwanda, hivyo sekta ya nyumba ina mchango mkubwa sana katika kuchochea ukuaji wa viwanda.
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 30,2018) wakati akizindua mradi wa Singidani Commecial Complex, mjini Singida. Jengo hilo la biashara na ofisi limejengwa na NHC kwa ajili ya kupangisha wafanyabiashara na taasisi mbalimbali.
Waziri Mkuu amesema sekta ya nyumba ni mtambuka kwa kuwa huchochea ukuaji wa uchumi, kutoa ajira na kukuza uwekezaji wa viwanda vya vifaa vya ujenzi kama saruji, mabati, nondo, marumaru na vinginevyo, ambavyo vinafungua fursa kubwa ya ukuaji wa viwanda.
Hivyo, Waziri Mkuu amesema wadau mbalimbali wanapaswa kuitazama sekta ya nyumba kama sekta mtambuka katika kuleta maendeleo endelevu ya uchumi na jamii kwa ujumla.
“Napenda kutoa pongezi kwa Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga jengo hili zuri na la kisasa kabisa hapa mjini Singida. Vilevile, jengo hili limeboresha na kupendezesha mandhari ya mji wa Singida kwa kiwango kikubwa kabisa,” amesema. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Jengo la Biashara la Singidani lililojengwa na Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC) mjini Singida Juni  30, 2018.  Watatu kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi. Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Felix Manyama Maagi na kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Neema Mgaya.  Wanne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida Juma Kilimba na wapili kulia ni Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kufungua Jengo la Biashara la Singidani lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) mjini Singida Juni 30, 2018. Kulia ni Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Juma Kilimba. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakimsikiliza, Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Margaret Ezekiel wakati alipotoa Maelezo kuhusu Jengo la Biashara la Singidani lililojengwa na NHC mjini Singida na kufunguliwa na Waziri Mkuu Juni 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wabunge walioshiriki katika ufunguzi wa Jengo la Biashara la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) la SIngidani mjini Singida Juni 30, 2018. Waliokaa, watatu kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, Wasita kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Juma Kilimba na  kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kufungua Jengo la Biashara la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini Singida, Juni 30, 2018.


Hivyo makala NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA

yaani makala yote NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/nhc-mna-jukumu-la-kuwafikia-watu-wa_30.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NHC MNA JUKUMU LA KUWAFIKIA WATU WA CHINI - MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...