Loading...
title : WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA
link : WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA
WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA
WAKINA mama 925,342 nchini wamefanikiwa kusajiliwa na mradi wa “Tumaini la Mama tokea ulipoanza mwaka 2012 na kuweza kunufaika huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga kilichofanyika mjini Korogwe.
Alisema idadi hiyo ni kuanzia mpango huo ulipoanza hadi mwezi Mei mwaka huu huku wakina mama wapatao 323,797 wakitokea mkoani Tanga pekee ambao wamesajiliwa.
Aidha alisema pia kaya 323.797 zimenufaika na kulipiwa fedha kwa ajili ya kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambapo sh.milioni 48,077,859,434 zimelipwa kwa watoa tokea mradi huo ulipoanza huku vituo vya mkoa wa Tanga vikilipwa kiasi cha sh.milioni 12,449,902,412.
“Pia vifaa tiba vyenye ya sh. milioni 900 vimenunuliwa na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma pia mradi umesaidia upatikanaji wa computers katika vituo vyenye mahitaji kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa kumbukumbu”Alisema.
“Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana mfuko utakaa na mfadhili kuona uwezekano wa kupata fedha zaidi kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi sisi viongozi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba mradi unatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili mfadhili aone umuhimu wa kuongeza muda zaidi”Alisema.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA
yaani makala yote WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/wakina-mama-925342-nchini-wasajiliwa-na_15.html
0 Response to "WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA"
Post a Comment