Loading...

WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA

Loading...
WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA
link : WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA

soma pia


WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA


Wanawake washiriki kujenga Wodi ya mama na mtoto - Chemba

Wanawake wa Kata ya Songolo, katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamejitoa katika ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto lililojengwa katika kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuchangia nguvukazi ili kupunguza changamoto za kutembea muda mrefu kutafuta huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho Bw. Saidi Msigwa mbele ya timu ya ukaguzi wa ujenzi wa vituo vya afya katika Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya mkoani Dodoma.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa Kata ya Songolo walijitokeza katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ndicho kilikuwa kilio chao cha muda mrefu cha kujengewa Wodi ya mama na Mtoto jambo lililopelekea wanawake wengi hasa wajawazito kwenda kujifungulia katika Hospitali ya Wialaya ya Kondoa.

Amesema kukamilika kwa Kituo cha afya cha Hamai kutasaidia wananchi wengi kupata huduma ya afya hasa vijiji vya jirani ambavyo ni Murongia, Itolwa , Jangalo, Jinjo, Kinkima na Kirerechangombena ambao wote hupata huduma katika kituo hicho.

Bw. Msigwa amesema mwaka 2015 wanawake wa Kata ya Songolo waliamua kijutolea kujenga jengo la Wodi ya Mama na mtoto kutokana na kuwepo kwa jengo moja la wodi ya Mama na Mtoto jambo ambalo lilikuwa likisababisha msongamano wa wamama wajawazito sababu hii ilipelekea wanawake kuamua kuchimba msingi na kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa wodi hiyo ndipo serikali ilipoamua kujenga jengo hilo mwaka 2018.

Bw. Msigwa ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga kituo cha afya cha Hamai ambacho kitasaidia wananchi maskini ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.Amesema kituo hicho kimejengewa wodi ya mama na mtoto, jengo la upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi ambapo mpaka sasa tayari zimetumika zaidi ya shilingi milioni 291.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Charles Kiologwe ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya chemba kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo yanaonyesha uhalisia wa matumizi ya fedha zilizotumika ukilinganisha na ubora wa majengo.

Aidha ameutaka uongozi wahuo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika maeneo ya karibu na wanapoishi.Naye Bi Martha Mariki Afisa afya Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ameutaka uongozi wa Halamashauri ya Wilaya ya Chemba kuhakikisha maeneo ya taasisi yanapimwa na kuwa na hati miliki, pia kuhakikisha wanaweka kwenye bajeti kama kipaombele cha kuweka uzio wa maeneo ya taasisi ili kuepusha maeneo mengi kuvamiwa na wananchi.
Jengo la Mama na Mtoto liliojengwa katika Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe akitoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima wakati walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.



Hivyo makala WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA

yaani makala yote WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/wanawake-washiriki-kujenga-wodi-ya-mama.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA"

Post a Comment

Loading...