Loading...

Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani

Loading...
Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani
link : Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani

soma pia


Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani

Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro Mhe. Sylvester Mabumba alikutana na kufanya mazungumzo na uongozi mpya wa Diaspora ya Watanzania waishio Komoro (TADICO) tarehe 23 Julai 2018. Viongozi hao wapya walifika ofisi za Ubalozi kwa ajili ya kujitambulisha ambapo miongoni mwa mambo waliyojadili ni pamoja na kutoa ahadi ya kuinua Diaspora ya Watanzania waishio Comoro ambapo kwa muda mrefu Diaspora hiyo imeonekana kuwa nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na Diaspora za nchi nyingine.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Mabumba alichukua fursa hiyo kuwapongeza viongozi hao wapya waliochaguliwa pamoja na kuwatakia kila la kheri katika nafasi zao hizo mpya walizoaminiwa na Watanzania wenzao. Aidha, Mhe. Mabumba alisisitiza juu ya umuhimu wa wanachama kulipa michango ya uanachama na vilevile kuwaomba viongozi kuwa wasimamizi wazuri wa matumizi ya fedha za wanachama hao.

Katika hatua za kuhuisha chama hicho wajumbe walishauriwa pia kuwa wabunifu katika mikakati yao na vilevile waangalie njia gani bora za kuibua vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea michango ya wanachama pekee. Pia Balozi Mabumba aliwahimiza viongozi hao kutosahau kuwekeza nyumbani na vilevile kuchangamkia fursa za biashara ambazo zinapatikana Tanzania na kuzitangaza Visiwani humo.
Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Balozi Sylivester Mabumba (kati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Ubalozi na viongozi wa Diaspora visiwani Comoro. Kutoka Kushoto ni Bw.. Hussein Banoga, Makamu Mwenyekiti; Bw.. Khamis Salum, Mweka Hazina; Bw.. Thabit Khamis, Afisa Ubalozi; Bw.. Fikiri Salum, Katibu Mkuu; Bw. Salum Ali, Mwenyekiti; Bw. Fuastine, Bw. Isakwisa na Bw. Mudrick Soragha. 
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja. 


Hivyo makala Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani

yaani makala yote Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/balozi-mabumba-awasisitiza-watanzania.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani"

Post a Comment

Loading...