Loading...

IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO

Loading...
IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO
link : IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO

soma pia


IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO

Na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaomba Viongozi wa dini nchini kuendelea kufanya doria za kiroho huku Jeshi hilo likiendeleza doria za kimwili kwa pamoja ili kuukabili uhalifu ikiwemo mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi ambayo yameanza kuongezeka katika siku za hivi karibuni.
IGP Sirro ameyasema hayo  kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Ukerewe na Sengerema mkoani Mwanza wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa Amani na utulivu.
Amesema Polisi wanafanya doria za kimwili ambazo wakati mwingine hutumia nguvu kushurutisha watu kutii sheria lakini Viongozi wa dini nao wana nafasi yao katika jamii kwa kufanya doria za kiroho na kukemea maovu.
IGP Sirro amesema makosa ya mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi yameanza kujitokeza kwa kasi katika siku za karibuni hivyo viongozi wa dini wana nafasi kubwa zaidi kuwaelimisha waumini wao kabla vifo havijatokea kwa kuwa wengi wao wanakuwa nao kila siku za ibada. 
Katika hatua nyingine IGP Sirro ameahidi kuchangia Shilingi milioni kumi na tano ili kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi katika  Kisiwa cha Kome, Wilayani Sengerema baada ya Wananchi kuomba kujengewa kituo hicho ili kukabiliana na uhalifu.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara Kisiwani Kome Wananchi hao walisema kujengwa kwa kituo hicho kutasaidia kuimarisha usalam katika maeneo hayo huku wakiomba kufufuliwa kwa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi.
IGP anaendelea na ziara yake huku akitumia usafiri wa Helkopta ili kujionea kwa uhalisia maeneo hayo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto za uhalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wakazi wa Kisiwa cha Kome Wilayani Sengerema mkoa wa Mara wakati wa Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. (Picha na Jeshi la Polisi)
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wakazi wa Wilaya ya Sengerema waliojitokeza kwa wingi kumlaki alipowasili Wilayani humo ikiwa kwa ajili ya kuendelea na Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akionyesha ukakamavu wakati wa kuimba na askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake mkoani humo ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasalimu viongozi wa dini kabla ya kuanza kikao nao Wilayani Serengeti ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na  viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Ukerewe baada ya kuwasili wilayani humo kuendelea na Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 


Hivyo makala IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO

yaani makala yote IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/igp-awaomba-viongozi-wa-dini-kuendeleza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO"

Post a Comment

Loading...