Loading...

WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI

Loading...
WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI
link : WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI

soma pia


WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

WAKAZI wa kata ya Tumbi, Kibaha Mjini mkoani Pwani ,wamelalamikia kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara kutoka Royal hospital hadi Mwanalugali na CCM Mkoa kuelekea shule ya Wipaz. 

Aidha, barabara ya kuelekea shule ya msingi Mwanalugali imekuwa mbovu hali inayosababisha wanafunzi kupata shida wakiwa wanakwenda shule. 
Akielezea juu ya changamoto ya baadhi ya barabara za ndani kuwa mbovu ,wakati wa muendelezo wa ziara ya jimbo inayofanywa na mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ,diwani wa kata ya Tumbi Hemed Chanyika alisema ufanyike uboreshaji wa barabara hizo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi. 

Akizungumzia suala la usafiri ,Chanyika alisema, walishafanya utaratibu wa kusogeza huduma hiyo ambapo kuna mabasi yanayofanya safari Mbezi -Mwanalugali lakini imejitokeza tatizo mabasi hayo kushindwa kuendelea na huduma hiyo hatua ambayo inawapa shida wakazi hao. 

Mkazi Hamis, Monika Mnyambirwa, Issa Gwaja, Shomari Gwaji walieleza, barabara hizo zinahitaji kuchongwa, mitaro ,madaraja ,kuwekwa matuta na makalavati.Akijibu juu ya kero hiyo, Koka aliitaka TARURA ihakikishe inakwenda kutatua kero hizo. 

Alielezea kwa mujibu wa TARURA barabara ya Royal hospital -Mwanalugali ipo kwenye mpango na mkandarasi atashughulikia tatizo hilo. "Suala la usafiri, miundombinu ya barabara ni muhimu katika jamii, kwani uinua maendeleo ya eneo husika "alisema Koka. Hata hivyo, Koka alibainisha ataendelea kushirikiana,kusimamia na kuwatumikia wananchi wa Mji wa Kibaha ili kutatua kero zinazowakabili.



Hivyo makala WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI

yaani makala yote WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wakazi-wa-kata-ya-tumbi-walalamikia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKAZI WA KATA YA TUMBI WALALAMIKIA KERO YA UBOVU WA BARABARA ZA NDANI"

Post a Comment

Loading...