Loading...
title : KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR
link : KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR
KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar amesema ushiriki wa Viongozi vijana wa Kiafrika Katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama ,Obama Foundation ni chachu kwa viongozi walioko madarakani kuendelea kuwamini kwa kuwapa nafasi za ju za uongozi .
Nassar ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita siku chache tangu ashiriki Kongamano lililoandaliwa na taasisi ya Obama Foundation na kuwashikisha vijana 200 kutoka mataifa 44 barani Afrika wanaofanya kazi serikalini ,asasi za kiraia na sekta binafsi ambao walikutana kwa muda wa siku tan katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Amesema katika Kongamano hilo kama vijana wamejifunza mambo mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yatachangia kujitokeza kwa vijana wengi zaidi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi watakaosaidia kuleta mabadiloko chanya katika bara la Africa.
Katika kongamano hilo lililoenda sambamba na sherehe za kilele cha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela,vijana nane kutoka Tanzania walichaguliwa kuiwakilisha nchi ya Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar akizungumzajambo na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama walipokutana nchini Afrika Kusini akiwa ni miongoni mwa Viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Afrika waliochaguliwa kushiriki Programu ya OBAMA AFRICA LEADERS PRORAM.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar kwa pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama wakiwajibika kwa kufanya kazi za mikono katika kuboresha miundombinu ya shule ya Far North School iliyopo pembezoni mwa jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Mbali na kushiriki kazi za mikono Rais Mstaafu wa Marekani,Barack Obama pia alipata nafasi ya kutoa mada katika kongamano lililowashirika viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Africa.
Wengine waliowasilisha mada katika Kongamano hilo ni pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Koffi Annan ,Rais wa Kwanza Mwananmke Barani Afrika na Rais Mstaafu wa Liberia ,Ellen Johnson Sirleaf
Hivyo makala KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR
yaani makala yote KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/kongamano-lililoandaliwa-na-rais-obama.html
0 Response to "KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR"
Post a Comment