Loading...
title : MKUU WA UPELELEZI ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI
link : MKUU WA UPELELEZI ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI
MKUU WA UPELELEZI ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI
*Ni katika kesi inayomkabili Halima Mdee
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MKUU wa Upelelezi Wilaya ya Ilala (RCO), Davis Msangi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hajawahi kumuhoji Rais John Magufuli jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yaliyotamkwa na mbunge wa Kawe Halima Mdee dhidi yake.
RCO Msangi ameyaeleza hayo leo mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipokuwa akijibu swali la Wakili wa utetezi Peter Kibatala.
Katika kesi hiyo, Mdee anakabiliwa na shtaka la kumtoa lugha chafu kwa Rais Dk. John Magufuli.
Akimuhoji shahidi huyo,Wakili Kibatala alimuuliza Msangi kama anamfahamu Rais John Magufuli na anaishi wapi. alijibu kuwa anaishi Ikulu. Pia alimuuliza shahidi huyo kama aliwahi kwenda kumuhoji jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mdee kwa sababu yeye ndiyo muhanga.
RCO Msangi alijibu kuwa hajawahi kwenda kumuhoji wala hakutumia taratibu zozote za kumuhoji.
RCO Msangi katika ushahidi wake amedai kuwa hafahamu msimamo wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na kauli ya Rais Magufuli kuhusu watoto wa kike waliopata mimba shule wasirudishwe shule.
Pia RCO Msangi alipoulizwa kwamba Mdee alikaa muda gani chini ya ulinzi, amedai kuwa sio kwa zaidi ya Saa 48, ambapo alifikishwa Polisi July 4,2018 ila tarehe kuondoka haijui.
Baada ya shahidi huyo kumaliza kuhojiwa na Wakili Kibatala, Hakimu Simba amesema kesi hiyo imeshatimiza mwaka mmoja na ilipaswa iwe ishatolewa hukumu, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi August 7 na 8, 2018 ili kuendelea na ushahidi.
Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa Julai 1 3 mwaka 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni ni kuwa Rais John Magufuli “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Hivyo makala MKUU WA UPELELEZI ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI
yaani makala yote MKUU WA UPELELEZI ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA UPELELEZI ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mkuu-wa-upelelezi-ilala-aulizwa-kama.html
0 Response to "MKUU WA UPELELEZI ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI"
Post a Comment