Loading...
title : NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO
link : NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO
NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO
Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
Nusu fainali ya kwanza ya Fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi inatarajiwa kuchezwa kesho kwa kuzikutanisha timi za Ubelgiji na Ufaransa.
Mchezo huo wa kwanza utakuwa ni muhimu kwa makocha wote wa timu mbili , Roberto Martinez wa Ubelgiji na Didier Deschamps wa Ufaransa.
Kwa upande wa Kocha wa Ufaransa Deschamps ameweka wazi mkakati wake wa kutaka kuweka rekodi ya kushinda taji hili akiwa meneja baada ya kuiongoza Ufaransa kushinda taji hilo mwaka 1998 akiwa nahodha wa kikosi cha dhahabu.
Deschamps atapambana na mchezaji mwenzie aliyekua katika kikosi hicho cha dhababu mwaka 1998 wakichukua ubingwa wa dunia Thiery Henry ambaye yupo kwenye benchi la ufundi la Timu ya Ubelgiji kwa sasa
Martinez kwa upande wake anaongoza kikosi chake ambacho kinatajwa kuwa na wachezaji wengi nyota katika historia ya soka la Ubelgiji.
Ebelgiji iliwaondoa Brazil katika hatua ya robo faainali kwa mabao 2-1 wakati Ufaransa iliinyuka Uruguay kwa mabao 2-0.
Hivyo makala NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO
yaani makala yote NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/nusu-fainali-ya-kwanza-ya-world-cup-ni.html
0 Response to "NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO"
Post a Comment