Loading...
title : TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO
link : TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO
TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unapenda kuwataarifu Waajiri wote Tanzania Bara na Umma kwa ujumla kwamba, huduma mpya ya uwasilishaji wa michango kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa malipo wa kielektroniki wa Serikali (Government Electronic Payment Gateway) inaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 1 Julai, 2018.
Huduma hii, pamoja na kurahisisha ulipaji wa michango, itamwezesha Mwajiri kupata stakabadhi ya kielektroniki na kumbukumbu za mtiririko wa michango yake.
Kutumia huduma hii, mwajiri atatakiwa kufungua akaunti ya mtumiaji kwa kuingia kwenye tovuti ya Mfuko (www.wcf.go.tz) na kubofya ‘‘on line services’’ (huduma za kimtandao).
Baada ya kufungua akaunti ya mtumiaji, Mwajiri atatakiwa kufanya yafuatayo;
1. Kuhakiki taarifa za Mwajiri pamoja na kuambatisha taarifa za Wafanyakazi;
2. Kulipa michango baada ya kupata namba ya udhibiti (control number) kupitia;
i. Benki za NMB na CRDB.
ii. Huduma za kifedha za mitandao ya simu kwa kupiga namba *152*00#.
iii. Njia ya kielektroniki ya kuhamisha fedha (Electronic Money Transfer) kutoka Benki anayotumia Mwajiri kwenda katika akaunti za Mfuko zilizopo NMB na CRDB.
Kwa mawasiliano zaidi tafadhali piga simu kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja (namba za simu ambazo ni bure 0800110028/0800110029) au tuma ujumbe wa barua pepe (helpdesk@wcf.co.tz). Aidha, Waajiri wote wanakaribishwa kutembelea banda la WCF lililopo katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl. J.K.Nyerere (Saba Saba) kwa wakati huu ambapo maonesho yanaendelea.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),
S.L.P 79655, Jengo la GEPF,
Barabara ya Bagamoyo,
DAR ES SALAAM.
Hivyo makala TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO
yaani makala yote TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/taarifa-kwa-waajiri-uwasilishaji-wa.html
0 Response to "TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO"
Post a Comment