Loading...
title : Tamasha la Mzanzibar Kurindima Wiki Ijayo Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. Tarehe 19-25/7/2018.
link : Tamasha la Mzanzibar Kurindima Wiki Ijayo Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. Tarehe 19-25/7/2018.
Tamasha la Mzanzibar Kurindima Wiki Ijayo Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. Tarehe 19-25/7/2018.
Na Mwashungi Tahir Maelezo.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mzanzibar ambapo linatarajiwa kufanyika tarehe 19-25 mwezi huu ambapo tamasha hilo hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa saba. .
Hayo amesema Katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Hassan Omar huko katika ukumbi wa mkutano ulioko Migombani wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utaratibu mzima utaofanyika wa tamasha la Mzanzibar linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Alisema tamasha hilo la 23 la Mzanzibar hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi huu kwa lengo kuu la kukuza mila , silka na utamaduni wa kizanzibar baada ya kuona vijana wetu wengi mambo ya zamani hawajui.
Pia alisema mambo mengi ya kizanzibar ya kiasili yamebadilika hivyo kufanyika kwa tamasha hili kutaweza kujulikana mambo mengi kwa vijana wetu ambapo walikuwa hawayajui zikiwemo ngoma za asili, vyakula na baadhi ya mambo mengine ya kiasili.
Aidha aliwaomba wananchi washiriki kwa wingi katika tamasha hilo litalofanyika katika Mapinduzi Square hapo Michenzani ambapo kutakuwa na fensi, kazi za mikono za wajasiriamali maulidi ya home na mambo mengi ya kiasili ambayo mpaka wageni wetu wa utalii watafurahishwa na mambo hayo.
Vile vile alisema pia tunashirikiana na kamisheni ya utalii hivyo wageni wetu watapata fursa ya kuona mambo ya kizanzibar ambayo huwavutia sana ambapo wazanzibar tunajivunia na mambo yetu ya kiutamaduni.
Alisema suala utamaduni ni muhimu ikiwemo lugha fasaha ya Kiswahili kwa kukizungumza na kuandika , aliomba tuikuze lugha yetu hii kwani kila siku Rais wetu anaipia kelele kwa lengo la kukithamini lugha yetu ya Kiswahili.
“Ni lazima tukienzi , tukithamini kwa kuandika , kuzungumza na hata kukitangaza Kiswahili chetu kwani Mh Rais wetu Dkt Ali Mohammed Shein anatuhimiza kudumisha matumizi ya Kiswahili sahihi” Alisema Katibu huyo.
Alieleza utamaduni unaporomoka hivyo tuache kuiga mambo yasiyofaa na kuyadumisha mambo yetu ya kiasili kwa lengo la kukuza mambo yetu ya kiasili .
Alifahamisha tamasha hilo pia litakuwa na taarabu asilia, kongamano la wasanii, mchezo wa Ngo’mbe ambao utafanyika Pemba na mabo mengi ya utamaduni wa kizanzibar yataweza kuonekana .
KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI UTAMADUNI NI NGAO KWA USTAWI WA MAISHA YETU.
MWISHO.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO.
Hivyo makala Tamasha la Mzanzibar Kurindima Wiki Ijayo Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. Tarehe 19-25/7/2018.
yaani makala yote Tamasha la Mzanzibar Kurindima Wiki Ijayo Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. Tarehe 19-25/7/2018. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tamasha la Mzanzibar Kurindima Wiki Ijayo Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. Tarehe 19-25/7/2018. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/tamasha-la-mzanzibar-kurindima-wiki.html
0 Response to "Tamasha la Mzanzibar Kurindima Wiki Ijayo Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. Tarehe 19-25/7/2018."
Post a Comment