Loading...
title : Umoja wa Ilala yetu wampongeza Rais
link : Umoja wa Ilala yetu wampongeza Rais
Umoja wa Ilala yetu wampongeza Rais
Viongozi wa Ilala yetu wakiwa katika Picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema Dar es salaam hivi karibuni wakati wa kumpongeza Rais John Magufuli, Katoka (kushoto)Vaileth Mbele ,Mohamed HONELO, MRATIBU wa ILALA Heri Shaban na Marysia Tukai(Picha na ILALA yetu)Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akipokea zawadi kutoka kwa Mohamed HONELO, hivi karibuni wakati Wana Ilala yetu walipokwenda kupeleka salam za pongezi kwa Rais kwa kuwatumikia wananchi wake katika Tanzania ya viwanda (Picha na Ilala yetu)
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Ilala yetu wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kwa utendaji wake wa kazi mzuri na kuongoza mapambano ya ukombozi wa Bara la Afrika kiuchumi.
Hayo yalisemwa na MRATIBU wa Ilala Yetu, Heri Shaban alipokwenda kupeleka salam za Rais kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala .
"Natumia nafasi hii kumpongeza Rais kwa utendaji wake wa kazi mzuri katika uongozi wake ameweza kuleta ndege ya nne Kati ya saba ameweza kusimamia Ilani ya chama vizuri katika Tanzania ya viwanda "alisema Shaaban.
Shaaban alisema kwa sasa nchi yetu imeweza kupiga hatua kiuchumi Rais Magufuli ameweza kusimamia miradi makubwa ikiwemo reli ya umeme .
Alisema jumuiya ya Ilala yetu itashirikiana na Serikali iliyopo madarakani katika kuleta Maendeleo,kutatua kero za Wananchi wa Wilaya ya Ilala na usimamiaji wa Ilani ya chama .
Aidha alisema umoja wa Ilala yetu ulianzishwa mwaka 2017 dhumuni lake kushirikiana kwa shida na raha,kushirikiana na Serikali kutatua kero mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameipongeza jumuiya hiyo kwa kutoa salam zao atazifikisha kwa Rais.
Mjema aliwataka wana Ilala kushirikiana na Serikali yao iliopo madarakani na kuunga mkono kazi za Rais.
Naye Mwananchi wa Ilala yetu,Mohamedi HONELO alisema Rais Magufuli ameweza kuitangaza nchi kwa kuipandisha nchi kimapato na uchumi wa viwanda.
HONELO alipongeza Serikali kwa kuboresha huduma za Afya katika hospitali zake ,pamoja na ukusanyaji mzuri wa mapato mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.
Hivyo makala Umoja wa Ilala yetu wampongeza Rais
yaani makala yote Umoja wa Ilala yetu wampongeza Rais Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Umoja wa Ilala yetu wampongeza Rais mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/umoja-wa-ilala-yetu-wampongeza-rais.html
0 Response to "Umoja wa Ilala yetu wampongeza Rais"
Post a Comment