Loading...
title : Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza
link : Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza
Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa washiriki wa mashindano ya urembo nchini kuzingatia maadili na tamaduni za kitanzania kwa kuwa kielelezo bora kwa jamii .
Hayo ameyasema jana Jijini Arusha wakati wa shindano la kumtafuta mrembwende wa Jiji hilo , yaliyoandaliwa na The Function House chini ya uongozi wa Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga yaliyoshirikisha warembo 19.
“ Ninyi ni kioo cha jamii, mnaangaliwa na jamii nzima hivyo msibweteke mnapopata umaarufu bali muwe kielelezo bora cha utamaduni na maadili ya Kitanzania ” amesema Mhe. Juliana Shonza . Anazidi kufafanua kuwa sanaa ya urembo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine,na kuwaomba wazazi na jamii kutoa ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha mabinti wanatimiza ndoto zao katika sanaa hiyo.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Jiji la Arusha, shughuli iliyoandaliwa na The Fuction House chini ya Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga jana Jijini hapo.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Katikati) akifuatilia matukio mabalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na washiriki wa urembo waliokuwa wanawania taji la Miss Arusha, jana katika ukumbi wa Lake Nyasa AICC, kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Bw. Kalisti Lazaro na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa The Fuction House Mrs. Chizenga.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (mwenye gauni la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa taji la Miss Arusha baada ya kumalizika kwa mashindano hayo jana Jijini hapo . Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza
yaani makala yote Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/washiriki-wa-urembo-zingatieni-maadili.html
0 Response to "Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza"
Post a Comment