Loading...
title : WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI
link : WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI
WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kununua madeni yaliyosababishwa na mikopo ya kibenki kwenye vyama vikuu vya ushirika nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.
“Serikali ya awamu ya tano hatuna biashara ya kununua madeni ya vyama vikuu, kulikuwa na tabia ya watu wa ushirika kukopa na hali ikiwa mbaya wanakimbilia Serikalini. Serikali hii hatuna biashara hiyo,” amesema.
Waziri Mkuu amesema anazo taarifa kwamba Chama Kikuu cha mkoa wa Kagera (KCU) kimekopa fedha Benki ili kiweze kulipa deni la mwaka 2014. “Nimeambiwa KCU wamekopa fedha benki ili kulipa deni la mwaka 2014, hii inaingia akilini kweli? Mnakopa fedha kulipa deni la zamani, ni kwa nini msiwatafute waliosababisha deni na kuwachukulia hatua?,” alihoji.
“Ninyi mlikuwa watu sita ambao mlikubaliana kama viongozi, mlienda kukopa kuzidi uwezo mlionao. Leo hii ni kwa nini serikali ije kulipa wakati mmetumia ninyi?,” aliuliza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya tatno inasisitiza masuala ya ushirika kwa sababu imeamua kuwahudumia wananchi kuanzia ngazi ya chini kuanzia pembejeo, dawa hadi masoko.
“Tunataka tuondoe utaratibu wa chama kikuu kukopa fedha benki ili kikanunue mazao. Vyama vingi vimetengeneza hasara, leo hii vyama vikuu vina madeni. Hii ni kwa sababu mlikopa fedha benki wakati hata hamjui mna kilo ngapi ambazo zimevunwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majalawa akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya ushirika dunianiyaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Julai 7, 2018.
Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akizungumza wakati alipomkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia katika Maadhimisho ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Julai 7, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Ushirika nchini, Bibi Renata Mwageni (kushoto) Tuzo ya Rais John Pombe Magufuli iliyotolewa na Wanaushirika nchini ili kutambua mchango wa Rais katika kuendeleza sekta ya ushirika na kuinua uchumi wa wananchi wa Tanzani ya 2018 . Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Juni 7, 2018. Wapili kushotoi ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika duniani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mizani ya Kielektroniki ya kupima uzito wa pamba wakati alipotembelea banda la Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza katika maonyesho ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwaanjelwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba iliyostawi vizuri wakati alipotembelea banda la Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama samaki waliokaushwa wakati alipotembelea banda la Vyma vya Ushirika katika Soko la Kimataifa la Kirumba – Mwaloni wilayani Ilemela baada ya kuhutubia katika Maadhimisho ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Zainab Telack na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa TANESCO wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI
yaani makala yote WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-serikali-haitanunua-madeni.html
0 Response to "WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI"
Post a Comment