Loading...

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE

Loading...
ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE
link : ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE

soma pia


ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE

Na Daniel Mwambene, Afisa Habari Ileje
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan   amewaonya Watanzania kutokufuru uumbaji wa Mwenyezi Mungu kwa kuharibu mazingira ili kuendelea kulinda ikolojia. 
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe katika kijiji cha Sange mara baada ya kuzindua shamba la miti la Iyondo-Mswima katika eneo la Katengele Mhe. Suluhu alisema kuwa kuharibu mazingira ni kumkufuru Mungu. 
“Kuharibu alichokileta Mungu kiwafae wanadamu huku mkiwa mnaenda misikitini na makanisani ni kumkufuru yeye”alisema kiongozi huyo. Alisikitishwa na shughuli za binadamu katika baadhi ya maeneo aliyoyapitia ndani ya wilaya ya Ileje ambako kilimo kinaendeshwa kando ya mito bila kujali sheria zinazolinda mito. 
Mhe.Suluhu alisema kuwa iwapo sheria hizo hazitazingatiwa iko hatari ya milima mingi kubaki vipara kwani kinachofanyika si ukataji miti kwa malengo ya kutunza akiba bali ni unyoaji wa miti. Aliongeza kuwa kamwe kilimo kisiwe kisingizio cha kuharibu mazingira kwakuwa uharibifu wa mtu mmoja huleta madhara kwa wengi. 
Awali kabla ya mkutano huo,Makamu wa Rais alizindua shamba la miti ambalo linaongeza idadi ya mashamba ya serikali huku likitarajiwa kutumia mamilioni ya pesa ambayo matokeo yake yataongeza ukubwa wa jina la Ileje kitaifa na kimataifa. 
Akitoa taarifa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndugu Joseph Mkude alisema kuwa wananchi wake ambao kwa asili ni wachapa kazi wamekuwa wakiitikia maagizo ya serikali vizuri ingawa wameonekana kufanya vibaya kwa kujiingiza katika imani za waganga wa jadi wajulikanao kama rambaramba. Viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiwemo machifu,wachungaji na vyama vya siasa ngazi ya mkoa wa Songwe waliiomba serikali kuendelea kutatua kero ya miundo mbinu ya barabra ili kuwaongezea kasi ya maendeleo wananchi ambao kwa sasa wanashuhudia ujenzi wa barabara ya Mpemba-Momba hadi Isongole-Ileje kwa kiwango cha lami.
 Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Sange
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan  akipanda mti eneo la Mradi wa upandaji miti la  Iyondo-Mswima Ileje.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan  akipata maelezo toka kwa Mohammed Kilongo Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi  Wakala wa Misitu(TFS).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akijiandaa kukata utepe wakati wa kuzindua shamba la miti la Iyondo-Mswima, Ileje


Hivyo makala ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE

yaani makala yote ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/ziara-ya-makamu-wa-rais-wilayani-ileje.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI ILEJE MKOA WA SONGWE"

Post a Comment

Loading...