Loading...
title : ASKARI MSTAAFU MBARONI KWA TUHUMA KUKODISHA SILAHA
link : ASKARI MSTAAFU MBARONI KWA TUHUMA KUKODISHA SILAHA
ASKARI MSTAAFU MBARONI KWA TUHUMA KUKODISHA SILAHA

Akizungumza jana Agosti 14, kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema watuhumiwa 39 wa matukio hayo walihusishwa kwenye matukio ya uhalifu ikiwamo kukutwa na silaha za aina tano, bangi kete 200, bangi misokoto 66, risasi 27, pamoja na pombe aina ya gongo lita 58.
Mtuhumiwa Lumi Guya maarufu kama Mbulu (67) mkazi wa Kingolwira alikamatwa kwa tuhuma za kukodisha silaha yake aina ya Shot Gun anayoimiliki kihalali kwa watu wanaofanya uhalifu.
Kamanda huyo amesema mtuhumiwa huyo ni mwanajeshi mstaafu wa JWTZ na hushirikiana na Miraji Jumanne(28)mkazi wa Kichangani ambaye inadaiwa aliwahi kuwa askari polisi na kufukuzwa kutokana na vitendo visivyofaa wakishirikiana na wenzao sita ambao wote wanashikiliwa.
Watuhumiwa wengine walikamatwa katika matukio ya wizi, uuzaji gongo, wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima na wizi wa kutumia silaha.
Hivyo makala ASKARI MSTAAFU MBARONI KWA TUHUMA KUKODISHA SILAHA
yaani makala yote ASKARI MSTAAFU MBARONI KWA TUHUMA KUKODISHA SILAHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASKARI MSTAAFU MBARONI KWA TUHUMA KUKODISHA SILAHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/askari-mstaafu-mbaroni-kwa-tuhuma.html
0 Response to "ASKARI MSTAAFU MBARONI KWA TUHUMA KUKODISHA SILAHA"
Post a Comment