Loading...

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA

Loading...
TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA
link : TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA

soma pia


TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA


Mwambawahabari
Ndugu wananchi,
Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yalianza rasmi mwaka 2003 baada ya Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika kuridhia kuwepo kwa sherehe hizo.  Maadhimisho haya hufanyika katika nchi 46 za kanda ya Afrika ambazo ni wanachama wa Shirika la Afya Duniani tarehe 31/08 ya kila mwaka.

Ndugu wananchi,
Tanzania, inaadhimisha maadhimisho haya kwa malengo makuu manne. Kwanza Tanzania ina nia ya kufufua ari na kujenga heshima ya huduma za tiba asili ambazo historia inatuambia kuwa zimekuwa zikikandamizwa na kudharaulika. Kwa kiwango kikubwa ukoloni pamoja na ukoloni mambo leo umekuwa ukikandamiza tiba zetu za asili na kufanya Waafrika wenyewe kuzinyanyapaa tiba hizo. Hali hiyo imetufanya tuyumbe, tukose dira na mwelekeo katika suala zima la kuboresha  Tiba Asili katika nchi yetu.

Pili kwa kupitia maadhimisho haya Serikali inawahamasisha Waganga wa Tiba Asili kujiepusha na migongano katika jamii kwa kutohusisha ushirikina na uchawi kama chanzo cha ugonjwa. Kuna taarifa  na migongano mingi ya kutisha juu ya hili.

 Itakuwa jambo la busara kwa waganga wa tiba asili kupitia kwenye vyama vyao kupanga mikakati ya kudhibiti na kuondoa kabisa vitendo vibaya vinavyochafua  taaluma yao.

Tatu, maadhimisho haya yanahimiza masuala ya uboreshaji na usajili wa dawa za asili. Lengo ni kuweza kutengeneza dawa kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya utengenezaji dawa bora.

Aidha  utafiti endelevu wa dawa za asili kwa magonjwa mbalimbali unahimizwa kwa madhumuni ya kupata dawa ambazo zinaweza kupatikana kiurahisi  ili mwenye kuhitaji aweze kuzipata.

Nne, kwa kupitia maadhimisho haya Waganga wa Tiba Asili wanahimizwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma na huduma za afya.

Ndugu wananchi,
Kama mnavyofahamu katika kuadhimisha Siku ya Tiba ya Asili ya Mwafrika kila mwaka tunakuwa na ujumbe maalum au kauli mbiu. Ujumbe maalum wa mwaka huu ni “Ujumuishaji wa Tiba Asili katika Mifumo ya Afya: Tulipofika sasa” (“Integration of Traditional Medicine in Health Systems: The journey so far”).

Kauli mbiu hii inawalenga na kutoa majukumu kwa Viongozi na Wataalam wa Tiba ya Kisasa kuweza kushirikiana na Waganga wa Tiba Asili katika utoaji wa huduma za afya. Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafanikiwa kuijumuisha huduma za tiba asili katika utoaji wa huduma za afya; Serikali imerasimisha huduma za tiba asili kwa kujumuisha katika Sera ya Afya; kuwepo kwa Sheria, Kanuni, Miongozo na taratibu za utoaji wa huduma za tiba asili nchini.

Aidha, Waganga wa Tiba Asili wanahimizwa kusajiliwa, kusajili vituo na dawa zao zinazotumika hususan dawa zinazouzwa katika maduka ya dawa za asili. Hadi tarehe 30 Juni, 2017; waganga 16,200; vituo 212 na dawa za asili tatu zimesajiliwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala. Huo ni mwanzo mzuri ijapokuwa juhudi zaidi zinahitajika kuwezesha “Ujumuishaji wa Tiba Asili katika Mifumo ya Afya: Tulipofika sasa”. Vilevile; nitoe wito kwa Waganga wa Tiba Asili kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu zinazowasimamia katika kutoa huduma za tiba asili kwa wateja wao.

 Nawataka wajiepushe na matangazo  yanayokizana na sheria, kanuni na taratibu ikiwa pamoja na kuondoa mabango yaliyozagaa mitaani yanayoonyesha kuwa wanaweza kutibu na kuponya magonjwa mbalimbali kwa mfano UKIMWI.

Ndugu wananchi,
Napenda kuwakumbusha wananchi kwamba kwa  sasa huduma za tiba asili zinatambuliwa rasmi kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Afya na Sheria namba 23 ya mwaka 2002. Madhumuni ya sheria hii ni kusimamia, kudhibiti na kuendeleza tiba asili ya Tanzania. Vilevile, udhibiti wa maadili ya uganga na ukunga wa tiba asili nchini umepewa kipaumbele.

Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Baraza la Tiba za Asili na Tiba Mbadala limeundwa kama chombo kikuu cha Serikali kitachosimamia na kuratibu shughuli hizo. Sheria hiyo  pia inalinda afya na haki za watum


Hivyo makala TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA

yaani makala yote TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/tamko-la-waziri-wa-afya-maendeleo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA"

Post a Comment

Loading...