Loading...
title : Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini
link : Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini
Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini
Na Jumia Travel Tanzania
Ushawahi kukumbana na kadhia ya kunyimwa huduma ya malazi? Au kulipishwa kwa kutozingatia masharti ya hoteli kuhusu huduma zao?
Wasafiri wengi siku hizi hufanya maandalizi ya mapema pindi wanapotaka kusafiri. Lengo la kufanya hivi linaweza kuwa kupata bei nzuri zaidi au kuepuka usumbufu wa maandalizi ya dakika za mwisho. Lakini kwa baadhi yetu, kufanya maandalizi ya namna hiyo huona kama ni kujisumbua tu kwa sababu kuna uwezekano wa kuahirisha safari yenyewe.
Unaweza kuona kuwa ni jambo la kawaida wewe kama mteja kuamua kuahirisha safari yako na kuwaambia hoteli wasitishe huduma ya malazi uliyoweka. Lakini kuna masuala muhimu ya kuzingatia kuhusu sera zinazowekwa na hoteli hususani katika kusitisha huduma ya chumba ambayo Jumia Travel ingependa kukupatia ufahamu.

Kuna umuhimu kwa wasafiri kuzifahamu sera za hoteli husika ukizingatia kumekuwa na mitandao mingi iliyoibuka kwa kasi katika utoaji wa huduma za malazi. Ushauri wa kwanza, msafiri anashauriwa pindi anapofikiria kusitisha huduma ya chumba hotelini aliyoifanya ni kujaribu kusoma kwa makini sera za hoteli ili kufahamu kwamba hatohitajika kulipia gharama zaidi pale atakapoamua kusitisha huduma.
Mambo muhimu ya kuzingatia
Endapo utakuwa umefanya huduma ya malazi ya chumba hotelini moja kwa moja utakuwa na faida mbili:
Kwanza, kama umeenda hotelini moja kwa moja na kufanya huduma kwa utaratibu uliozoeleka unaweza kuwa na faida ya kusitisha huduma yako hata masaa 24 kabla ya kuripoti. Utaratibu huu unaweza kukupa faida ya kurudishiwa takribani pesa zako zote kama ulishalipa au hautokatwa chochote kama hautokuwa umelipa. Mara nyingi njia hii ni rahisi na huwa haina matatizo.
Pili, kama utakuwa umefanya huduma ya malazi ya kabla basi ujue suala la kusitisha huduma kwako litakuwa ni changamoto kwako. Hii ni kutokana na sababu ya kwamba kwa mtazamo wa hoteli, utakuwa umepewa ofa ya bei nzuri tofauti na wengine na hawatokuwa tayari kukuachia uende kirahisi. Ukiachana na kufanya huduma ya malazi moja kwa moja hotelini, siku hizi kuna njia za kufanya huduma kupitia mitandao mbalimbali.
Mfumo wa kufanya huduma za malazi kwa njia ya mtandao unakupatia fursa ya kuperuzi na kulinganisha huduma za hoteli mbalimbali kwa urahisi na wakati mmoja. Faida ya kutumia mitandao kama hii ni kwamba mingi miongoni mwao huonyesha sera za hoteli katika kusitisha huduma ya malazi uliyoifanya.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>
Hivyo makala Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini
yaani makala yote Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/athari-zinazoweza-kukukumba-kwa.html
0 Response to "Athari zinazoweza kukukumba kwa kusitisha huduma ya malazi hotelini"
Post a Comment