Loading...
title : DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018
link : DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018
DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018
Na Frankius Cleophace, Tarime
KATA ya Nkende iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara katika kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka 2018 imetumia zaidi ya Sh.milioni 458 katika utekelezaji wa miradi mbalimbaliya Maendeleo.
Baadhi ya miradi hiyo ni ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara huku wananchi wakichangiazaidi ya Sh.milioni 22.Wakati Diwani wa kata hiyo Daniel Komote akichangia zaidi ya Sh.milioni 15 kwa lengo la kutekeleza miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuunga juhudi za Serikali.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata hiyo Komote katika kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kata ya Nkende Mjini Tarime.
Komote amesema kuwa amekuwa akishawishi wananchi katika kuchangia maendeleo kupitia sekta zote bila kujali itikadi za vyama ili wananchi waweze kuondokana na adha ambao wamekuwa wakipata kutokana na ukosefu wa huduma za muhimu karibu, likiwemo suala la Afya, Elimu, na Miundombinu ya Barabara na Maji.
Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote akifafanua mambo yaliyofanyika kipindi cha Januari mpaka Juni 2018 katika kata yake kupitia sekta ya Afya,Maji,Elimu, Miundombinu ya Barabara na Masuala ya kijamii.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka Kura akisisitiza jambo katika kikao hicho baada ya diwani wa kata hiyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kata ya Nkende Mjini Tarime.
Wajumbe wa kamati ya Siasa kata ya Nkende wakiwa katika kikao hicho cha kuwasilisha taarifa ya ilani ya chama hicho ngazi ya kata.
Baadhi yawageni wakiwemo Madiwani kutoka kata mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.
Hivyo makala DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018
yaani makala yote DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/diwani-kata-ya-nkende-mjini-tarime.html
0 Response to "DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018"
Post a Comment