Loading...
title : JPM AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KING MAJUTO
link : JPM AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KING MAJUTO
JPM AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KING MAJUTO
Na, Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaongoza watanzania kutoa heshima za mwisho kwa gwiji wa sana nchini Majuto ambaye alifariki Agosti 8 mwaka katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mwili wa marehemu mzee Majuto umewasili katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam, huku wasanii mbalimbali wa vichekesho, maigizo, pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na serikali waliofika katika viwanja hivyo wameonekana kwa majonzi.
Viongozi wa waliofika kutoa heshima ya mwisho ni Rais Dkt. Magufuli, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu wa Waziri Habari, Sanaa na Michezo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
Kwa upande wa wasanii asilimia kubwa wameungana katika kuhakikisha wanamsindikiza Msanii mwezao katika safari ya mwisho.
Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na JB, Mr Cheni, Mwanalisa na wengine wengi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti vyama vya wasanii pamoja na viongozi mbalimbali wamesema kuwa mzee Majuto ameacha pengo kubwa katika tasnia ya sanaa kwa ujumla na hakuna mtu anayeweza kuliziba.
Wamesema kuwa wamejifunza mambo mengi lakini kubwa ni upendo wake pamoja umoja alionyesha katika kipindi chote cha uhai wake.
Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda mkoani Tanga ambapo unatarajia kuzikwa kesho.
Hivyo makala JPM AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KING MAJUTO
yaani makala yote JPM AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KING MAJUTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JPM AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KING MAJUTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/jpm-aongoza-mamia-ya-watanzania-kutoa.html
0 Response to "JPM AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KING MAJUTO"
Post a Comment