Loading...

MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII

Loading...
MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII
link : MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII

soma pia


MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, amewaondoa wasiwasi wanachama wa mifuko minne inayounganishwa, wadau wote wa sekta ya hifadhi ya jamii na wananchi, kwamba serikali imelifanya jambo hilo kwa umakini mkubwa.

Pia amesema hatua ya serikali ya kufanikiwa kuunganisha mifumo hiyo inatakiwa kupongezwa hasa baada ya nchi nyingi kushindwa kutekeleza.

Mhagama ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kufungua semina ya wahariri na waandishi wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Mhagama amesema serikali imehakikisha kwamba michango, mafao, rasilimali na uwekezaji wa mifuko inayounganishwa inaendelea kuwa salama kwa maslahi ya wanachama na nchi kwa ujumla.

Amesema wanachama wote ikiwa ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko iliyounganishwa ambayo ni PSPF,LAPF,PPF na GEPF watahamishiwa katika Mfuko wa PSSSF, hivyo haki na stahili zao zitaendelea kutolewa na mfuko huo bila kuathiri kwa namna yoyote ile.

Mhagama amesema vivyo hivyo, watumishi wote wa mifuko iliyounganishwa watahamishiwa katika mfuko mpya ambako uongozi wa mfuko huo utawapangia majukumu yao kwa kuzingatia muundo wa mfuko huo.

"Rasilimali, vitega uchumi, madeni, mifuko ya hiyari na mikataba iliyokuwa chini ya mifuko iliyounganishwa itahamishiwa katika mfuko wa PSSSF,"alisema.

Mkurugenzi Mkuu SSRA, Dk Irene Isaka, alisema hatua hiyo ya uunganishwaji wa mifuko imelenga kupunguza gharama za uendeshaji na kuondoa ushindani usio na tija baina ya mifuko hiyo.

Aidha alibainisha kuwa taratibu za utambuzi na uhakiki wa uwekezaji na rasilimali za mifuko umefanyika na kwa sasa Wizara ya Fedha na Mipango iko katika uhakiki wa rasilimali za mifuko iliyounganishwa.

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Jesse Kwayu alisema wapo waliostaafu kuanzia mwaka jana mwishoni na mpaka leo hawajapata mafao yao.

"Hivyo kupitia mkutano huu wanatarajia watapata taarifa kuhusiana na uchewaji huo wa kupatiwa mafao,"tunategemea tukitoka hapa tutakuwa na ujumbe mzuri,"amesema Kwayu.

Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Onorius Njole alisema pia viwango vya uchagiaji bado vitabaki pale pale ambayo ni asilimia tano kwa mfanyakazi na 15 kwa mwajiri na kuwa hakutakuwa na fursa ya mwajiriwa kuchangia zaidi ya asilimia 10



Hivyo makala MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII

yaani makala yote MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mhagama-awatoa-hofu-wanachama-mifuko-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MHAGAMA AWATOA HOFU WANACHAMA MIFUKO YA JAMII"

Post a Comment

Loading...