Loading...
title : NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI
link : NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI
NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA
Baada ya kuyapandisha hadhi mapori matano ya akiba, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kuwekeza katika Mapori hayo.
Aidha, Amesema Serikali imefuta kodi ya kuingiza magari ya watalii nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi kuingia katika biashara hiyo ikiwa lengo ni kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya Utalii. Ametaja aina ya uwekezaji unaohitajika kuwa ni ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya nyota moja hadi zenye nyota tano, nyumba za kulala wageni, uanzishwaji wa makampuni ya utalii pamoja na kutoa huduma za vyakula kwa ajili ya watalii.
Ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Karagwe mkoani Kagera kabla ya kutembelea ziwa Ngoma ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyopo katika Pori la Akiba la Kimisi ambalo ni miongoni mwa mapori yaliyo katika mchakato wa kuwa hifadhi za taifa.
Naibu waziri huyo anatembelea mapori ya mkoa wa Kagera kufuatilia hatua iliyofikiwa na Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA)katika kuyaendeleza. Amesema Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika ni hazina na fursa kwa mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kufunguka kiutalii kwa wananchi wa maeneo hayo na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa ramani inayoonesha Ziwa Ngozi ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika Pori la Akiba la Kimisi na aliyekuwa Meneja wa Pori hilo Bigilamungu Kagoma wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngala pamoja na baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU)
Hivyo makala NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/naibu-waziri-hasunga-awaita-wawekezaji.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI"
Post a Comment