Loading...
title : ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI
link : ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI
ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuhudia wananichi wa mkoa wa Mwanza wakiteketeza zana haramu wakizozisalimisha katika ziara yeke ya kuhamasisha ufungaji samaki kwa vizimba katima Ziwa Victoria.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafanyabiashara na wavuvi katika soko la samaki la kimataifa Kirumba jiji Mwanza ambapo amewaomba kulipa kodi ili kuongeza patato la taifa.
Maibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza wakikagua miundombinu ya soko la samaki kimataifa la Kirumba.
Sehemu ya wavuvi pamoja na wafanya biashara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.
Na Leandra Gabriel, Glob ya jamii.
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza Maafisa uvuvi kuweka hadharani tozo za samaki pamoja na mazao ya uvuvi kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo.
Ulega amesema hayo leo katika soko la samaki la kimataifa la Kirumba jijini Mwanza wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya mifugo na uvuvi.
Ulega ameeleza kuwa viongozi husika lazima wajue na kutambua majukumu yao bila kusubiri Waziri kuja kukagua maendeleo ya masoko. Na amewataka na maafisa na wafanyabiashara kukaa na kupanga mikakati ya kuongeza mapato ya Serikali.
Aidha ameagiza kuwa masoko yote ya samaki yaweke wazi tozo ambazo mfanyabiashara anatakiwa kulipa pindi wanunuapo bidhaa.
Pia Naibu Waziri amewataka Maafisa kutembelea masoko kila wiki ili kujua maendeleo ya masoko, Kuhusu udhibiti wa uvuvi haramu Ulega amewapongeza wavuvi kwa kutii sheria bila shuruti kwani hakuna nyavu haramu iliyokamatwa katika ukanda wa ziwa Viktoria na Kayenze.
Pia amewashauri wafanyabiashara kujua tozo wanazotakiwa kutoa kabla ya kununua mizigo kwani itawasaidia sana katika ufanyaji wao wa biashara kwa kutambua kiasi wanachotakiwa kulipa kama tozo kuliko kutoa tozo bila kujua nj kiasi gani wanatakiwa kulipa.
Kwa upande wao wavuvi pamoja na wafanyabiasha ra wameishukuru serikali kwani kwa sasa samaki wanapatika tofauti na mwaka jana na wamewataka maafisa kushirikiana nao ili kuweza kufikia malengo ya juu zaidi.
Hivyo makala ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI
yaani makala yote ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/ulega-aagiza-tozo-za-samaki-na-mazao-ya.html
0 Response to "ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI"
Post a Comment