Loading...

NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO

Loading...
NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO
link : NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO

soma pia


NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa J.K Nyerere uliopo Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MOCu) kwa ajili ya kufungua mkutano wa Tano wa chama hicho.

Na Dixon Busagaga,Moshi.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) kimeiomba serikali kutunga sera ya uwepo wa eneo rafiki la kulelea au kunyonyeshea watoto katika sehemu za Kazi pamoja na kuunda chombo cha kusimamia utekelezwaji wa uwepo wa sera ya unaynyasaji wa kijinsia katika taaasisi za elimu ya juu nchini.

Mbali na ombi hilo THTU pia kimewasilisha ombo kwa serikali la kuundwa Vyombo vya kufuatilia waajiri ambao hawazingatii maagizo ya sera zinazotungwa na serikali ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi sambamba na uwepo wa muundo wa utumishi kwa wafanyakazi waendeshaji katika taasisi za umma za elimu ya juu nchini.
Hayo yalibainishwa wakati wa mkutano mkuu wa tano wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ukishirikisha zaidi ya wanawake 80 kutoka vyuo vikuu 36,vitatu vikiwa ni vya binafsi na 33 vya serikali . 
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi ,iliyosomwa na katibu wa THTU,Amina Mdidi ,wanawake hao walisema THTU imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kutokuwepo kwa mwongozo wa mishahara au bodi ya kusimamamia na kudhibiti malipo ya watumishi kwa vyuo binafsi.

“Changamoto nyingine zinazootukabili ni baadhi ya taasisi kutolipa nauli za likizo kwa enza wa wafanyakazi wanawake (Mume) na watoto chini ya miaka mitano na ukosefu wa vituo rafiki kwa malezi ya watoto wachanga”alisema Mdidi.

Katika hatua nyingine ,Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania kilitoa ripoti ya utafiti juu ya utekelezaji wa sera ya maendeleo ya mwananmke na jinsia ya mwaka 2000 katika taasisi za elimu ya juu Tanzania ikionyesha aslimia 80 ya taasisi hizo zilionyesha kutokuwepo kwa masuala ya jinsia katika mpango mkakati wa taasisi.

Baadhi ya Wajumbe wakiwa katika mkutano huo.

Akisooma utafiti huo ,Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake (THTU) taifa Salma Fundi alisema asilimia 80 ya taasisi hazikuonyesha uwepo wa mafunzo kwa wanafunzi au wafanyakazi kuhusiana na masuala ya jinsia.

“Asilimia 70 ya taasisi hazina sera ya unyanyasaji wa kijinsia ambazo ni muhimu katika kupunguza ubaguzi wa kijinsia na ukatili huku asiliamia 60 ya washiriki walikuwa na mtazamo hasi juu ya sera ya jinsia kwa kuamini ni sera inayomhusu mwanamke tu”alisema Fundi.

Katika hotuba yake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo,Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa alisema THTU kwa muda mfupi kimekuwa chama kinachotoa chachu ya maendeleo na amani ndani ya taasisi za elimu ya juu Tanzania. 



Hivyo makala NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO

yaani makala yote NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/naibu-waziri-stella-ikupa-afungua_16.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO"

Post a Comment

Loading...