Loading...

Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni

Loading...
Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni
link : Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni

soma pia


Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni


Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar                  

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico  amezindua Mabaraza ya Wazee ambapo kwa kuanzia Mabaraza hayo yatafanya kazi katika Jimbo la Magomeni.

Kuundwa kwa mabaraza hayo kunakusudiwa kuwaweka pamoja 
Wazee hao na kuanzishiwa miradi ya ujasiri amali ya kuendeleza maisha yao na kuondokana na umasikini.

Akizindua Mabaraza hayo katika uwanja wa Meya Waziri Castico ameitaka Jamii Wazee ipasavyo na kuheshimu mawazo yao kwani ndio hazina kubwa kwa Familia na Taifa kwa ujumla.

Amefahamisha kuwa Wazee wana haki ya kutoa mawazo yao na kusikilizwa kutokana na kujua vitu vingi na uzoefu unaotokana na umri mkubwa na utumishi wao.

Waziri Castico amesema Wazee hao wametumika muda mwingi katika kazi mbalimbali Sekta binafsi na Serikali ikiwemo Uhasibu na Nyanja mbalimbali za ulinzi hivyo mawazo yao ni muhimu.

Aliongeza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amewapa kipaumbele katika Serikali yake na huwapa pencheni ya kila mwezi ili kujikimu mahitaji yao bila ubaguzi.

Amesisitiza kuwa Wizara yake iko makini katika kuhakikisha wazee wote wanakuwa na mazingira mazuri ya kuwapatiwa mambo muhimu yanayohitajika ikiwemo matunzo ya uhakika na malezi bora.

“Wizara yangu iko mstari wa mbele kwa kuwalinda wazee kwani wao ndio wenye fikira na busara katika kupanga mambo ya maendeleo yao” .Alisema Waziri huyo.

Hata hivyo aliwasihi wazee hao kuzidisha mashirikiano na kusaidia kuweka mikakati ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimekithiri katika jamii.

Sambamba na hayo viongozi wa jimbo hilo akiwemo mbunge Jamal Kassim Ali na Mwakilishi Rashid Makame Shamsi wameahidi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wazee hao na kuwapatia huduma za afya.

Viongozi hao pia wameahidi kuwa karibu nao na kupokea fikra na busara zao kwa kwa faida yao na Jimbo kwa ujumla.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR


Hivyo makala Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni

yaani makala yote Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/waziri-castici-azindua-mabaraza-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Castici azindua Mabaraza ya Wazee jimbo la Magomeni"

Post a Comment

Loading...