Loading...
title : BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI
link : BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI
BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI
Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MSIMU wa Tisa wa mashindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS) umezinduliwa rasmi ikishirikiana na Kampuni ya Startimes jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wanawapongeza BSS kwa kukuza vipaji toka msimu wa kwanza mpaka msimu huu ujao ambao unatarajia kuruka hewani hivi karibuni kupitia Startimes Swahili .
Malisa ameeleza mipango yao kushirikiana na Bss kuhakikisha inakuza vipaji na kunyanyua vijana kuonyesha vipaji vyao, pia kipindi hiki ni chenye maudhui na kinaweza kutazamwa na rika zote .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark production ambae pia ni Jaji Mkuu Ritta Paulsen ameiomba Serikali kuangalia na kutoa mchango kwenye sekta ya muziki kwani inaongeza Pato la Taifa na wasanii wamekua wakiendesha maisha yao kupitia muziki.
Hivyo amesema katika msimu huu wanaomba ushirikiano kwa watanzania wote kwani wanaamini hiki ni kipindi kinachofatiliwa na watu wengi sana kwa hiyo vijana wajitokeze kuonyesha vipaji vyao.
Kuhusu ratiba ya usahili itakua mikoa mbalimbali kamaMwanza, Dar es salaam, Arusha, Mbeya na usahili huo utaanza Septemba na kauli mbiu ikiwa ni Jiongeze piga hatua.
Wakati huo huo mmoja wa wasanii ambao wameibuka baada ya kuibuliwa na BSS Kala Jeremaya amewapongeza Benchmark kwa kulirudisha shindano hilo na kueleza mafanikio ambayo amepata.
Amesema kwani amekua akishirikiana na watu wakubwa kutoka mashirika mbalimbali kutokana na fursa ambayo amepata kutoka kwenye shindano na kumtambulisha vizuri na kumpa fursa kujulikana kwa urahisi zaidi huku akiendesha maisha yake kupitia muziki wake.
Uongozi wa Startimes Tanzania pamoja na uongozi wa Bongo Star Search wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa
shindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS).
Uongozi wa Startimes Tanzania pamoja na uongozi wa Bongo Star Search wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa
shindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS).
Hivyo makala BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI
yaani makala yote BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/bongo-star-search-yazinduliwa-rasmi.html
0 Response to "BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI"
Post a Comment