Loading...
title : INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA
link : INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA
INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA
Na Said Mwishehe,Globu ya kamii
KIVUKO cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani
Ukerewe mkoani Mwanza kimezama ziwa Victoria.
Inadaiwa kwamba kivuko hicho kimezama kikiwa na abiria ambapo hata hivyo bado haijafahamika idadi ya abiria waliokuwemo ingawa taarifa za awali zinadai kilikuwa na abiria zaidi ya 90.
Kwa mujibu wa baadhi ya waliozungumzia kivuko hicho wamedai sema kilikuwa kinatokea Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye ghati ya Ukara.
Kwa mujibu wa nashuhuda wamedai kuwa ghafla kilianza kutitia kwenye maji kwa nyuma kulikokuwa na mzigo na kuwezesha abiria waliokuwa mbele kurukia majini na kuogelea na mitumbwi iliyokuwa pale kufanya kazi ya kuwaokoa abiria waliorukia majini.
Pia inadaiwa abiria wengi waliokuwa ndani ya Mv Nyerere hawakuweza kutoka na kuwa wamezama.
Mmoja ya waliozungumzia kiazama kwa kivuko hicho amedai idadi yaabiria waliopanda haijulikani ingawa uwezo wa kivuko ni kubeba abiria 150.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo hazikifanikiwa kwani simu yake haikuwa hewani.
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada y kupigiwa simu ya mkononi alisema yupo kikaoni.
Hivyo tutaendelea kuwajuza kinachoendelea na idadi kamili ua abiria waliokuwamo kwenye kivuko hicho.
Wakati huo huo Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ambayo chini ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano umesema unasikitishwa na tukio la kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere.
Kivuko hicho kimekuwa kinatoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Ukara na Bugolora wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari naKitengo cha Habari na Mawasiliano cha TEMESA imesema wanasikitishwa na ajali hiyo na inawaomba wananchi wote kuwa na subira wakati taarifa zaidi kuhusu tukio hilo la kusikitisha zikiendelea kutolewa.
Hivyo makala INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA
yaani makala yote INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/inasikitishakivuko-cha-mvnyerere.html
0 Response to "INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA"
Post a Comment