Loading...
title : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited.
link : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya uzalishaji wa matairi ya vyombo vya moto ya Futang Group Limited, kutoka Nchini China walipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati katik akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya uzalishaji wa Matairi ya Vyombo vya Moto ya Futang Group Limited yenye Makamo Makuu yake Shanghai Nchini China.Ujumbe huo unaongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Tang Biao wa Pili kutoka Kushoto, wa kwanza Kushoto ni Katibu wake Bwana You Feiteng na wa kwanza kutokja Kulia ni Katibu Muhtasi wao Kampuni Bibi Zhang Ying.
Picha na OMPR
Na.Othman Khmais .OMPR.
Kampuni ya Kimataifa ya utengenezaji wa Mipira ya Gari ya Futang Group Limited kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China imeonyesha nia ya kutaka kujenga kiwanda cha Kutengeneza Matairi ya Gari, Baskeli na vyombo vyengine vya Maringi Mawili Visiwani Zanzibar ili kulihudumia soko la Tanzania pamoja na Ukanda wa Afrika Mashariki.
Uamuzi wa Kampuni hiyo umekuja Wiki moja tu baada ya Tanzania kutangaza fursa wa Uwekezaji ilizonazo katika Maonyesho ya 15 ya Kimataifa ya Biashara ya China - Asean Expo 2018 yaliyofanyika wiki iliyopita katika Mji wa Nanning ndani ya Jimbo la Guangxi Nchini China.
Nia ya kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Futang Group Limited Bwana Tang Biao aliyeuongoza Ujumbe wa Viongozi Watatu wa Kampuni hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Tang alisema Kiwanda cha Kampuni hiyo kimeshapata uzoefu wa kutengeneza matairi ya Vyombo vya usafiri katika mazingira ya kutopata pancha hata iwapo mipiRa hiyo itapambana na misumari mingi zaidi wakati chombo kinapokuwa katika safari zake za kawaida bara barani.
Alisema Wataalamu wa Kiwanda hicho tayari wameshayafanyia majaribio matairi yanayozalishwa kwa takriban miaka 13 sasa ambapo mpira hata kama utapata misumari mara 200 bado utakuwa na uwezo wa kutembea bila ya kuleta athari yoyote.
Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya Futang Group Limited alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Tairi linalozalishwa na Kapuni hiyo lina uwezo wa kutembea katika kipindi cha Miaka Miwili hadi Mitatu hata kwenye kwenye bara bara zisizokuwa katika kiwango.
Alieleza kwamba Uongozi wa Kampuni yake uko tayari kutoa mualiko kwa Wataalamu wa ufundi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenda kuangalia harakati za uzalishaji za kiwanda hicho kwa lengo la kujiridhisha kutokana na umakini wa Bidhaa zake.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umekuja na Habari njema yenye nia ya kutaka kulitumia Soko la Tanzania katika Uwekezaji wa Viwanda vyao.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kutoa msaada wowote utaohitajika kwa Uongozi wa Kampuni hiyo katika azma yake ya kutaka kuwekeza Miradi yao Visiwani Zanzibar ambayo kwa umuhimu wake itasaidia kutoa huduma ndani ya Soko la Afrika Mashariki.
Alifahamisha kwamba Sera ya Uwekezaji iliyopo Nchini hutoa punguzo la Kodi kwa Mali Ghafi zinazotolewa Nje ya Nchi kuzipatia Kampuni au Taasisi zitakazoazimia kuanzisha Miradi yao ya Kiuchumi na Biashara hapa Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Kampuni hiyo kuandika Maombi na kuyawasilisha kwa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} ili kuchukuliwa hatua zitakazofaa katika kuona malengo ya nia yao yanafanikiwa.
Hivyo makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited.
yaani makala yote Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar-mhe_58.html
0 Response to "Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited."
Post a Comment