Loading...

MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI

Loading...
MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI
link : MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI

soma pia


MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wachimbaji madini katika mgodi wa  dhahabu wa Mwabomba
Mchimbaji mdogo wa madini  aliyefahamika kwa Jina la Sungwa Chalamila (30-40) mkazi wa Nywarwerwe Bulungwa amefariki dunia baada ya kuporomokewa na kifusi cha udongo na Matimber (Magogo) katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa dhahabu Mwabomba kijiji cha Mwabomba kata ya Idahina tarafa ya Dakama Halmashauri ya Ushetu wilaya Kahama mkoa wa Shinyanga. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule aliyefika eneo la tukio amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia  Septemba 11,2018 majira ya saa saba na nusu katika duara namba moja kwenye mgodi wa Mwabomba. 

Amesema Sungwa Chalamila alifariki dunia baada ya kuporomokewa na kifusi cha udongo na magogo akiwa chini mita 100 katika shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu huku wenzake watatu wakijeruhiwa. 

Kamanda Haule amewataja watu ambao wamepata majeraha mbalimbali mwilini katika tukio hilo kuwa ni Sagoda Yuda,Richard Elias na Mlekwa Sai ambao wameokolewa kwa kushirikiana na jeshi la polisi, wachimbaji wadogo wa eneo hilo na jeshi la Zima Moto na Uokoaji la Halmashauri ya Mji wa Kahama.

"Majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Kahama kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri",alieleza Kamanda Haule. 

Ameongeza kuwa tukio hilo limetokea katika duara namba moja linalomilikiwa na wanachama wanne ambao ni Sengerema Yahururuka,David Jaba Masai Said na Masoud Ramadhan.


Hivyo makala MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI

yaani makala yote MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/mchimbaji-madini-afariki-dunia-baada-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MCHIMBAJI MADINI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPOROMOKEWA NA KIFUSI"

Post a Comment

Loading...