Loading...
title : Watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa ujangili wa meno ya Tembo wafikia 17
link : Watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa ujangili wa meno ya Tembo wafikia 17
Watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa ujangili wa meno ya Tembo wafikia 17
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
WATUHUMIWA wa mauaji ya Mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya Tembo sasa wamefikia 17 baada ya leo Septemba 10.2018 mshtakiwa mwingine raia wa Burundi kusomewa mashtaka yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Hamisi Ali , mshtakiwa Habonimana Nyandwi raia wa Burundi ameunganishwa leo na kusomewa mashtaka mawili ya kula njama ya kufanya mauaji na mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilis hi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la Palms Foundation, Wayne Lotter (52).
Washtakiwa wengine ambao walishasomewa mashtaka yao ni raia wa Burundi, Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) mkazi wa Kamenge Burundi, Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A. Inocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini. Meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B, Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B na Mohammed Maganga (61) mchimba makaburi.
Wengine ni, Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Ayoub Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie,
Washtakiwa wote hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ambapo katika shtaka la kwanza wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Lotter.
Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni Dar es Salaam walimuua Lotter.
Washtakiwa wote wako rumande kwa kuwa kesi ya mauaji inayowakabili haina dhamana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 17.2017 kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wake bado haujakamilika.
Hivyo makala Watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa ujangili wa meno ya Tembo wafikia 17
yaani makala yote Watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa ujangili wa meno ya Tembo wafikia 17 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa ujangili wa meno ya Tembo wafikia 17 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/watuhumiwa-wa-mauaji-ya-mwanaharakati.html
0 Response to "Watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa ujangili wa meno ya Tembo wafikia 17"
Post a Comment