Loading...
title : VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA
link : VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA
VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA
VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA KWENYE KUPIMA UZITO PALE SOKO LA VETENAL LILIOPO TAZARA KUKUTANA KATIKA MASUMBWI SEPTEMBA 15 TAIFA.
Na Mwandishi Wetu
Haidari Mchanjo Katika ali isiyokuwa ya kawaida kwa mashabiki wa michezo baada ya kucheza mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama Ndondo Cup sasa timu za Goms United na Keko Furniture zinakutana katika masumbwi ambapo Goms united inawakilishwa na bondia Haidari Mchanjo na Keko Furniture anatoka Fred Sayuni
mashabiki wa mabondia hawo wamepanga kuanza shangwe zao siku ya ijumaa wakati wa kupima uzito kwenye soko la vetenal lililopo maeneo ya Tazara Dar es Salaam kuanzia saa nne na watacheza jumamosi katika uwanja wa ndani wa Taifa 'Indoor Stadium'
Mabondia pamoja na kambi zao watapima uzito ijumaa na watacheza siku ya jumamosi ambapo kwa sasa yameshafanyikamaandalizi ya kutosha kwa mabondia wote kilichobaki ni mpambano tu kufanyika
Akizungumzia pambano hilo mratibu wa mapambano ya ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka kampuni ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi wakati Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atazipiga na Geoger Dimoso na Vicent Mbilinyi atavaana na Saidi Mpoma 'Kidedea' wakati Mohamedi Kashinde atakumbana na Sadiki Momba na Imani Daudi ataoneshana umwamba na Paul Kamata.
Na mpambano mwingine utawakutanisha Faraji Sayuni na Issa Nampepeche Ramadhani Shauri atakumbana na Said Amani wakati Mwinyi Mzengela atakumbana na Kassimu Rajabu 'Boxer Mnyama' Saidi Zungu na Tonny Rashidi Super D aliongeza kwa kusema kuwa mapambano hayo yote yataanza kuanzia saa 12 jioni ili zimalizike kwa wakati
mapambano hayo yameandaliwa na kampuni ya ngumi za kulipwa ya Super D Boxing Promotion inayoendelea kuinuwa vipaji vya mabondia mbalimbali nchini ili kujikuzia kipato na kujiweka nafasi nzuri kwa mabondia kucheza kila wakati
Hivyo makala VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA
yaani makala yote VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/vigoma-vya-keko-furniture-na-goms.html
0 Response to "VIGOMA VYA KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED KUANZA IJUMAA"
Post a Comment