Loading...
title : VIJANA 8140 WA MBAGALA WAOMBA UTARATIBU KUPATIWA KADI ZA CCM, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI
link : VIJANA 8140 WA MBAGALA WAOMBA UTARATIBU KUPATIWA KADI ZA CCM, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI
VIJANA 8140 WA MBAGALA WAOMBA UTARATIBU KUPATIWA KADI ZA CCM, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
KATIKA kuelekea kuadhimisha miaka mitatu ya uongozi wa Rais John Magufuli vijana kutoka kata za Mbagala wakiwa na kauli ya "Jamii Mpya" wametuma salamu za pongezi na kumtakia afya njema ya mwili na akili kwa Rais na wameomba utaratibu katika ngazi za kata na Wilaya ili waweze kujiunga na CCM.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Dar live, mratibu wa shughuli hiyo Ally Makwilo ameeleza kuwa tamasha hilo ni la kumpongeza Rais Magufuli kwa nguvu na juhudi katika kujenga jamii mpya na wanamuamini sana katika suala la uongozi na kutenda haki na wamemshukuru katika juhudi zake za utoaji wa elimu bure, ujenzi wa viwanda, kupiga vita rushwa, ufisadi na usawa.
Kuhusiana na vijana kutaka kujiunga na Chama cha Mapinduzi, Makwilo amesema kuwa vijana 8140 kutoka Mbagala wanaomba utaratibu wa kujiunga na chama hicho ili waweze kuwa nae pamoja katika ujenzi wa taifa na amewaasa vijana kutumia fursa ya elimu inayotolewa bure katika kutimiza malengo yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa hafla hiyo Joyce Mbena amesema kuwa malengo ya kongamano hilo yamelenga pia kuwafanya vijana kutambua nafasi yao kuanzia na yale ambayo serikali inafanya kwa ajili yao.
Aidha amewataka viongozi wengine bila kujali itikadi ili kuweza kulifikisha taifa mbali zaidi na pia wao kama vijana wapo bega kwa bega na wamehaidi kushirikiana nae katika ujenzi wa taifa kwani wao ni jamii mpya.
Aidha vijana hao wameeleza kuwa hawapo tayari kusikia wala kuona Rais akidhihakiwa au kutoa maneno ya kejeli kwani amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mratibu wa tamasha la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli Maendeo Allya Mamwilo akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja
Sehemu ya vijana waliofika kwenye tamasha la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli lililo fanyika leo Mbagala jiji Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Hivyo makala VIJANA 8140 WA MBAGALA WAOMBA UTARATIBU KUPATIWA KADI ZA CCM, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI
yaani makala yote VIJANA 8140 WA MBAGALA WAOMBA UTARATIBU KUPATIWA KADI ZA CCM, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA 8140 WA MBAGALA WAOMBA UTARATIBU KUPATIWA KADI ZA CCM, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/vijana-8140-wa-mbagala-waomba-utaratibu.html
0 Response to "VIJANA 8140 WA MBAGALA WAOMBA UTARATIBU KUPATIWA KADI ZA CCM, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI"
Post a Comment