Loading...
title : Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka
link : Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka
Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka
Na.WAMJW,Bungeni,Dodoma
Idadi ya wanachama wachangiaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imeongezeka kutoka wanachama 164,708 waliokuwa wameandikishwa mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 mwezi Septemba 2018.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma.
“Ongezeko hili limetokana na kanuni na misingi inayotumika katika kuendesha utaratibu wa mfuko huu ikiwa ni pamoja na uchangiaji wenye usawa kwa kuzingatia viwango vya mshahara,usawa katika kupata huduma na ushiriki wa Serikali katika usimamizi kwa faida ya wanachama” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa kwa upande wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), jumla ya kaya zilizojiunga hadi Septemba mwaka huu ni 2,220,953 ikiwa ni sawa na wanufaika wapatao 13,506,330 sawa na asilimia 25 ya watanzania wote’ kwa hiyo mifuko hii yote inatoa huduma kwa watu 17,656,697 sawa na asilimia 33 ya watanzania wote kwa mujibu wa idadi ya makadirio ya watanzania kwa sasa.Idadi ya wanufaika imeongezeka kutoka 691,774 mwaka 2001/2002 hadi wanufaika 4,150,367 sawa na asilimia 8 ya watanzania wote” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka sasa idadi ya wanachama wengi waliojiunga asilimia 67 ni watumishi wa umma ambao wanajiunga kwa mujibu wa sharia.
Hata hivyo Waziri Ummy alisema mfuko unaendelea kutoa elimu na kubuni vifurushi mbalimbali vitakavyovutia wananchi wengi kujiunga na kufaidika na mfuko ambapo utawawezesha wanachama wengi zaidi kujiunga hasa wale wa sekta isiyo rasmi na kujiwekea malengo ya kuwafikia watanzia asilimia 50 mwaka 2020.
“Mfuko umekamilisha uandaaji wa vifurushi vya michango na mafao kulingana na uwezo wa wananchi kulipia bima ya afya,suala hili lipo katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kwa utekelezaji”. Alisisitiza Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa mpango huo utamwezesha mwananchi kuchagua vifurushi vya aina mbalimbaliu vya huduma anayoitaka kwa utaratibu utakaojulikana kama ‘JIPIMIE’ na wanachama watalipa kidogo kidogo kwa utaratibu ujulikanao kama ‘DUNDULIZA’ ambao tayari umeshakamilika.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijinini Dodoma ambapo alisema wachangiaji wa mfuko huo wameongezeka kutoka wanachama 164,706 mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 septemba mwaka huu.
Mkurugenzi wa NHIF Bw.Bernad Konga akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa kamati ambapo alisema mfuko wake upo tayari kuanza mara moja kutoa huduma kupitia vifurushi vipya vitakavyojulikana kama JIPIMIE ili watanzania waweze kupata huduma za matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini
Wakurugenzi wa NHIF wakipitia taarifa ya mfuko huo wakati ikiwasilishwa kwenye kamati mapema leo
Katibu Mkuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya(wa kwanza kulia),Mkurugenzi wa NHIF Bw.Benard Konga(anayefuata)pamoja na wakurugenzi wengine wa Wizara na NHIF wakifuatilia taarifa hiyo.
.WazirinUmmy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
Hivyo makala Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka
yaani makala yote Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/idadi-wa-wachangiaji-wa-mfuko-wa-bima.html
0 Response to "Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka"
Post a Comment