Loading...

MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII

Loading...
MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII
link : MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII

soma pia


MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII

 Na Lydia Churi-Kwimba Mwanza 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakumbusha  Majaji na Mahakimu kutumia Mamlaka waliyonayo kisheria kutoa adhabu zinazoirekebisha jamii kwa makosa yanayojirudia mara kwa mara.
Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kwimba leo Jaji Mkuu alisema Mahakama ni sehemu ya jamii hivyo inalo jukumu la kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwa amani na salama.
Kuhusu ushirikiano kati ya Mahakama na mihimili mingine, Jaji Mkuu alisema katiba ya nchi imegawanya majukumu kwa kila mhimili lakini yote inaunganishwa  na dhana moja ya kuwatumikia wananchi, hivyo aliahidi kuendeleza ushirikiano na wadau wote ili wananchi wapate haki kwa wakati.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama haiwezi kufanya kazi peke yake bila kushirikiana na mihimili mingine. “Nguvu ya Mahakama inatokana na nguvu kutoka kwenye mihimili mingine”, alisema.  
Awali akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi  Ngaga alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao hulazimika kukatisha masomo yao.
Kuhusu ushirikiano na Mahakama, Mkuu huyo wa wilaya alisema ofisi yake inashirikiana kwa karibu na Mahakama katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.
Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake katika mkoa wa Mwanza ambapo anakagua shughuli za Mahakama. Tayari ameshatembelea baadhi ya Mahakama zilizopo kwenye  wilaya za Ukerewe, Sengerema na Kwimba.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za kimahakama wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Happyness Ndesamburo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na viongozi wengine wa Mahakama pamoja na Mahakimu wa Mahakama zilizopo wilayani Kwimba mara baada ya kuzungumza nao.
.Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga pamoja na Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Mansoor Shanif Hiran.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kwimba baada ya kuzungumza nao leo katika ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika.




Hivyo makala MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII

yaani makala yote MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/majaji-na-mahakimu-wakumbushwa-kutoa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII"

Post a Comment

Loading...