Loading...

MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF

Loading...
MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF
link : MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF

soma pia


MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF


MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo ameipongeza Benki ya NMB nchini kwa juhudi zake za kuendelea kuukuza mchezo wa Golf Tanzania.

Jenerali Mabeyo ametoa pongezi hizo jana kupitia kwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed alipokuwa akimwakilisha katika hafla ya kufunga Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Jenerali Mabeyo, Luteni Jenerali Mohamed alisema jamii ya mchezo wa Golf Tanzania inatambua mchango mkubwa unaotolewa na NMB katika kudhamini mchezo huo mara zote jambo ambalo linaendeleza kukua kwa mchezo huo nchini, hivyo wataendelea kushirikiana na benki hiyo.Alisema NMB wamedhamini mashindano hayo kwa mwaka wa tatu mfululizo huku yakizidi kukua na mchezo huo kuwa maarufu nchini, na yamekuwa yakishirikisha wachezaji vijana na wameanza kufanya vizuri jambo ambalo ni mafanikio kwa taifa kimichezo.

Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa NMB alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na jamii katika kuendeleza na kukuza michezo yote pale inapopata fursa kwani mbali ya kujenga mahusiano mazuri na jamii pia ni afya na sasa ni sehemu ya ajira kwa jamii. Alisema NMB itaendelea kushirikiana na Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo kwani ni shukrani kwa mahusiano waliyonayo kikazi.

Mgeni rasmi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed (wa pili kulia) kwenye Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi mchezo wa Golf akimkabidhi kikombe mshindi wa jumla katika mashindano hayo, Richard Mtweve (kulia). Kutoka kushoto wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara NMB, Donatus Richard, Mwenyekiti wa Klabu ya Golf Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo. 
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed akizungumza lipokuwa akiyafunga Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam. 
Mshindi wa jumla katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf, Richard Mtweve akizungumza kwa furaha mara baada ya kupokea vikombe vya ushindi. 



Hivyo makala MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF

yaani makala yote MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/mkuu-wa-majeshi-jwtz-aipongeza-nmb.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF"

Post a Comment

Loading...