Loading...

RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO

Loading...
RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO
link : RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO

soma pia


RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ameagiza kukamatwa kwa waliokuwa viongozi wa Soko la Kimataifa Kariakoo kwa kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3.
Vigogo walioagizwa kukamatwa ni aliekuwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya utumishi, mkuu idara ya manunuzi na aliekuwa mkuu idara ya mipango na biashara ambao wameagizwa kufikishwa mahakamani Mara moja. RC Makonda ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa utatuzi wa kero za wafanyabiashara Soko la Kariakoo ambapo pia ametoa siku tano kwa watendaji kupitia upya sheria zote za ushuru mdogomdogo baada ya kubaini uwepo wa ushuru mkubwa unaoumiza na kuwarudisha nyuma wafanyabiashara. 
"Hatuwezi kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha Nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo 600, ushuru wa Siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyohuyo analipa ushuru wa Choo na Bafu 500, hili haliwezekani" Alisema RC Makonda. 
 Aidha RC Makonda ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa makusanyo ya ushuru baina ya mbia na soko na badala yake ameagiza kazi ya ukusanyaji wa ushuru ifanywe na uongozi wa soko.
Pamoja na hayo RC Makonda ameagiza soko kuu la Kariakoo kurejeshwa kwenye hadhi ya kimataifa na sio kuendeshwa kiholela kama ilivyo sasa ambapo linapokea bidhaa za rejareja kutoka mitaani badala ya kuwa soko la kuuza bidhaa za jumla. 
 Miongoni mwa kero zilizolalamikiwa na wafanyabiashara ni uhusiano mbovu baina ya viongozi na wafanyabiashara, kodi ya pango, vyanzo vingi vya ushuru, mikataba, mikopo, soko kupoteza mwelekeo, mkanganyiko kwenye viwango vya vipimo, kadi ya kizimba na ukamataji ambapo RC Makonda ameahidi kuzifanyia kazi.



Hivyo makala RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO

yaani makala yote RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/rc-makonda-aagiza-kukamatwa-kwa-vigogo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO"

Post a Comment

Loading...