Loading...

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA

Loading...
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA
link : SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA

soma pia


SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya halmashauri ya wilaya ya Lushoto.

Amesema lengo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye uwezo wa kutoa huduma mbalimbali muhimu zikiwemo za maabara, upasuaji na mama na mtoto.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Oktoba 31, 2018 wakati akizungumza na wakananchi katika kata ya Malindi, baada ya kutembelea jengo la soko mbogamboga la Malindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika sekta ya afya baada ya bajeti ya kununulia dawa kuongezeka kutoka sh. bilioni 31 kwa mwaka na kufikia bilioni 269.

“Hatutaki tena kusikia mgonjwa anaenda hospitali na kukosa dawa biashara hiyo tumeimaliza, Rais Dkt. John Magufuli ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa.”

Amesema katika wilaya ya Lushoto Serikali imetenga sh. bilioni 1.4 kwa ajili ujenzi na ukarabati wa majengo ya vituo vya afya vya kata za Kangagai. Mnazi na Mlola.

“Halmashauri wekeni mpango thabiti wa kujenga wodi mbili kati yake moja ya wanaume na nyingine ya wanawake, lengo la Serikali ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi.”

Aizungumzia kuhusu mradi wa ujenzi wa soko, Waziri Mkuu amesema mradi huo ni sehemu ya huduma zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii nchini.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto  akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga Oktoba 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge wakati alipotembelea ofisi mpya za Halmshauri hiyo baada ya kuzindua jengo la utawala, Oktoba 31, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la mbogamboga na matunda linalojengwa na Serikali katika kijiji cha Malindi wilayani Lushoto, Oktoba 31, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.  Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Oktoba 31, 2018. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lukozi katika Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga,  Oktoba 31, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA

yaani makala yote SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/serikali-imedhamiria-kuboresha-huduma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...