Loading...
title : TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU YADHAMIRIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
link : TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU YADHAMIRIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU YADHAMIRIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
Na Mwandishi Wetu- Arusha
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imeadhimiria kupambana na vitendo vya ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni kwa kuzalisha wataalamu wa maendeleo ya jamii ambao watasaidia kutoa elimu na kuhamasisha jamii ili kuondokana na ukatili huu wa kijinsia ambao kwa kiasi kikubwa humkosesha haki mtoto wa kike katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George wakati akifungua mdahalo wa siku moja uliofanyika Chuoni hapo wenye lengo la kujadili changamoto ziwapatazo watoto wa kike na kusababisha kukatiza ndoto zao kuelekea mafaniko ya kimaisha.
Aidha Mkuu huyo wa Chuo aliwataka washiriki wa mdahalo huo kujadiliana kwa uwazi ili kutoa fursa kwa washiriki wa mdahalo huo kupata elimu sahihi ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike na kuwa kikwazo kwao kufikia ndoto zao kielimu lakini pia kutoa fursa kwa wanafunzi wa chuo chake kutambua namna bora kukomesha vitendo vya ukatili kwa kuwa itakuwa jukumu la kiutendaji kwa kwakuwa wao ni wataalamu wa maendeleo ya Jamii.
Dkt. Bakari amesema kuwa vijana ni waathirika wakubwa wa mimba na ndoa za utotoni ikiwemo tatizo la ukeketaji hususani katika mikoa ambayo inaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni na ukeketaji tatizo ambalo kimsingi linatokana na mila na desturi potofu hapa nchini.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakary George akifungua mdahalo wa kujadili masuala ya Mimba na Ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Bw. Christopher Mushi akieleza lengo la mdahalo kwa wajumbe wa mdahalohuo uliojadili masuala ya Mimba na Ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.
Wadau na wanafunzi mbalimbali wakifuatilia kwa makini mdahalo wa kujadili masuala ya Mimba na Ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano- WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU YADHAMIRIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
yaani makala yote TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU YADHAMIRIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU YADHAMIRIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/taasisi-ya-maendeleo-ya-jamii-tengeru.html
0 Response to "TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU YADHAMIRIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI"
Post a Comment