Loading...
title : WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE
link : WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE
WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE
WAGONJWA wa macho 379 wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wamepatiwa huduma ya vipimo na matibabu ya macho bure kwenye maadhimisho ya siku ya macho duniani.
Katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu wa afya kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ‘Kilimanjaro Center for Community Opthmology ( KCCO) kupitia mradi wa (TRACHOMA SAFE) wametoa huduma ya kupima macho, ushauri, kutoa dawa sambamba na kuwapangia tarehe ya kurudi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na upasuaji wagojwa ambao wameonekana kwamba matatizo yao ya macho yanahitaji upasuaji.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto Dkt Malkiadi Paschal Mbota alisema ugonjwa wa Trakoma ni tatizo kubwa na idara ya Afya kwa kushirikiana na KCCO wamekuwa wakienda katika maeneo yote ya vijijini kutoa hudumaza ushauri, dawa, upasuaji, kutoa elimu juu ya umuhimu wa kusafisha uso kwa maji safi pamoja na usafi wa mazingira kwa ujumla kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo.
Dkt Mbota alitoa wito kwa jamii, hususani jamii ya kifugaji kujenga tabia ya kunawa uso kwa maji safi mara kwa mara ili kuepuka ugonjwa wa Trakoma. “Mikakati ya wilaya katika kukabiliana na ugojwa huo, kwa kushirikiana na KCCO tumekuwa tukienda kijiji hadi Kijiji kuwatambua wagonjwa na tukishawatambua, madaktari wetu na manesi wamejengewa uwezo wa kutosha kuwapatia huduma zote zinazotakiwa ikiwemo upasuaji, wanaweka mahema hukohuko vijijini wanawafanyia upasuaji,” alisema.
Mkazi wa eneo la Kibaya Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, akipatiwa maelezo ya matibabu bure ya ugonjwa wa macho.
Mganga wa macho wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, akimpima macho mkazi wa mtaa wa Kaloleni, Juma Ally.
Mganga wa macho wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, Dk Enock Awary akimpima macho mkazi wa Kibaya, Khadija Hamis ambapo watu 379 walipatiwa vipimo na matibabu bure
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kibaya Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, walio na matatizo ya macho wakipewa maelezo ya namna ya kupata matibabu.
Hivyo makala WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE
yaani makala yote WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wagonjwa-wa-macho-379-kiteto-watibiwa.html
0 Response to "WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE"
Post a Comment