Loading...
title : WALIMU TABORA WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA WA ELIMU NAMBA 24 WA 2002 WAKATI WA KUTOA ADHABU YA VIBOKO
link : WALIMU TABORA WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA WA ELIMU NAMBA 24 WA 2002 WAKATI WA KUTOA ADHABU YA VIBOKO
WALIMU TABORA WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA WA ELIMU NAMBA 24 WA 2002 WAKATI WA KUTOA ADHABU YA VIBOKO
NA TIGANYA VINCENT
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu amewataka walimu katika shule mbalimabli mkoani humo kuzingatia Waraka wa Elimu namba 24 wa mwaka 2002 wakati utoaji adhabu za viboko kwa wanafunzi ili kuepuka kuingia katika matatizo na kushitakiwa kwa makosa mbalimbali.
Alisema lengo ni kuhakikisha wanapotoa adhabu za viboko kwa wanafunzi watukutuku wanazingatia matakwa ya Waraka huo na kuepuka kuingia tuhuma za kushitakiwa kwa makosa ya jinai kama yaliyotokea hivi karibuni mkoani Kagera.
Makungu ametoa kauli hiyo jana wakati wa kikao kazi cha siku moja na Maafisa Elimu Kata, Walimu wa wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kutoka Wilaya ya Tabora, Wilaya ya Uyui na Sikonge ili kuwapitisha katika mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi wao.
Alisema kuna baadhi ya walimu wanasifika kwa utoaji wa adhabu ya viboko jambo ambalo ni hatari kwao na kwa ajira zao na familia zao.
“Hivi walimu wenye tabia ya kupenda kuchapa viboko vingi kinyume cha maagizo ya waraka huu…wanafanya hivyo hivyo na kwa watoto wao au ni sawa na usemi usemao mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu”aliuliza.
Makungua alisema walimu wanadhamana kubwa ya kuwafundisha na kuwalea watoto kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi ili hatimaye waje kuwa viongozi na watumishi wema wa nchi hii.
Alisema Waraka huo unaeleza vizuri namna ya utoaji wa adhabu ya viboko izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsi, afya ya mtoto na visizidi vinne kwa wakati mmoja na kutaka mtoto wa kike adhibiwe na Mwalimu wa Kike labda kama hakuna.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(katikati) akitoa ufafanuzi juu ya walimu kuzingatia Waraka wa Elimu namba 24 wa mwaka 2002 kuhusu adhabu ya viboko. Ametoa ufafanuzi huo jana wakati wa kikao kazi cha siku moja cha Maafisa Elimu Kata na Walimu wa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari kwa Wilaya za Tabora , Uyui na Sikonge. Wengine kwenye picha ni Katibu Tawala Msaidizi(ELIMU) Susan Nussu(kulia) na Afisa wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora Shukuru Kazembe(kushoto)
Baadhi ya Maafisa Elimu Kata na Walimu wa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari kutoka Wilaya za Tabora , Uyui na Sikonge wakiwa katika kikao kazi cha siku mjini Tabora jana kilichowaelimisha mambo mbalimbali ikiwemo uzingatiaji wa araka wa Elimu namba 24 wa mwaka 2002 kuhusu adhabu ya viboko.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WALIMU TABORA WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA WA ELIMU NAMBA 24 WA 2002 WAKATI WA KUTOA ADHABU YA VIBOKO
yaani makala yote WALIMU TABORA WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA WA ELIMU NAMBA 24 WA 2002 WAKATI WA KUTOA ADHABU YA VIBOKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WALIMU TABORA WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA WA ELIMU NAMBA 24 WA 2002 WAKATI WA KUTOA ADHABU YA VIBOKO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/walimu-tabora-watakiwa-kuzingatia.html
0 Response to "WALIMU TABORA WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA WA ELIMU NAMBA 24 WA 2002 WAKATI WA KUTOA ADHABU YA VIBOKO"
Post a Comment