Loading...
title : WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI
link : WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI
WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.
Chama cha waajiri nchini ATE wamefanya Mkutano wa pamoja kwa kukutana na wanachama na wafanyakazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waajiri ATE Dr Aggrey Mlimuka amesema sheria mpya ya waajiri iliyotolewa Agosti Mosi mwaka huu imebainisha taratibu zote za kujiunga na mifuko hiyo.
Amesema kuwa, kwa upande wa waajiri wanatakiwa kuhakikisha waajiriwa wao wanajiunga na mifuko hiyo ya kijamii NSSF,GEPF na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF ili kupata haki na wajibu .
Kaimu Katibu wa Mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya jamii SSRA Joseph Mutashubilwa ameeleza lengo la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha kila mfanyakazi anajiunga na mifuko hiyo ya NHIF,PSPF,GEPF na kupitia upya sheria iliyoanza kutumika rasmi mwaka huu mwezi Agosti ambayo Ina mamlaka ya kusimamia mifuko ya jamii.
Aidha , Mutashubilwa amesema fursa waliyopata waajiriwa katika elimu hiyo wataweza kusambaza kwa waajiri wao ili kuhakikisha wanapata haki zao bila changamoto yoyote japo kumekuwepo kwa tatizo la waajiri hao kupangiwa sehemu za kupata huduma za kiafya na kulazimika kwenda mbali na maeneo ambayo wanayoishi.
Ametoa fursa kwa wanachama hao kuwasilisha malalamiko yao katika ofisi zao zilizopo Dar es salaam, Dodoma au kutuma barua pepe.
Katika hafla hiyo Mwanachama wa ATE ambae ni Meneja rasilimali watu kutoka kampuni ya PSSI Hollyness Mongi ametoa ufafanuzi kwa mifuko hiyo kuungana na kuwa chini ya SSRA.
Mongi ameshukuru Mkutano wanachama walikua Kwenye sintofahamu kutokana na Mabadiliko ya utaratibu wa mifuko hiyo kuungana na kupelekea wafanyakazi wapya kutojua taarifa sahihi ya kujiunga na mifuko hiyo upya.
Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha Waajiri nchini ATE Dr. Aggrey Mlimuka akizungumzana na wadau pamoja na waajiri katika hafla fupi ya kutambulisha sheria mpya ya Mifuko ya pensheni jijini Dar es Salaam
Kaimu Katibu wa Mamlaka ya udhibiti wa Mifuko ya pensheni nchini (SSRA) Joseph Mutashubilwa akizungumzana na wadau kuhusu kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.
Meneja rasilimali watu kutoka kampuni ya PSSI Hollyness Mongi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sheria mpya kwa Waajiri pamoja na waajiriwa kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama na wafanyakazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.
Hivyo makala WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI
yaani makala yote WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wanachama-na-wafanyakazi-nchini.html
0 Response to "WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI"
Post a Comment