Loading...

AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

Loading...
AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
link : AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

soma pia


AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

Na Khadija Seif blogu ya Jamii

MCHEZA  video Rutyfiya Abubakari maarufu kwa jina la Amber Ruty (23), Said Bakari Mtopali (21) (kijana wake AmberRuty) na kijana anayedaiwa kuwa Shoga maarufu, James Charles Mpali a.k.a James Delicious(22) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Washtakiwa hao ambao wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wamesomewa mashtaka yao leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Wakili wa Serikali Nguka Faraji.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Katuga amedai katika shtaka la kwanza linalomkabili AmberRuty peke yake, kuwa, kabla au Oktoba 25 mwaka huu katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alimruhusu mshtakiwa Mtopali kumuingilia kimwili kinyume na maumbile.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa Mtopali anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile na AmberRuty.Aidha, mshtakiwa Delicious anadaiwa kuchapisha na kusambaza video za kingono kupitia kompyuta kosa analodaiwa kulitenda kati au Oktoba 25, 2018 akiwa katika sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam.Anadaiwa, siku hiyo alisambaza video za ngono zisizokuwa na maadili kupitia mtandao wa kijamii  wa WhatsApp

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ambapo wanadaiwa kati Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kwel.Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana

Kabla ya kusomwa kwa masharti ya dhamana Wakili Katuga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wanasubiri taarifa za Kitaalamu kutoka kwa daktari na statement kutoka kwa mashahidi juu ya picha hizo za ngono za minato. Katika masharti ya dhamana, Mahakama imewataka washtakiwa kuwa kila mmoja kuwa na wadhamini 2 waliotakiqa kusaini bondi ya Sh. Milioni 15.

Pia wadhamini wametakiwa kuwa na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zeo za kusafiria na pia hawaruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam bila ruksa.Hata hivyo ni mshtakiwa James Delicious pekee ndiye aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana, huku Amber Ruty na Said Bakary Mtopali wameshindwa kutimiza masharti na kupelekwa gerezani.Kesi hiyo imeahirishwa hadi November 12,2018.
MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty)  pamoja na James Charles maarufu kama James Delicious anayedaiwa kuwa shoga wakielekea kwenye moja ya chumba cha Mahakama mara baada ya kufikishwa   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.


Hivyo makala AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

yaani makala yote AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/amber-ruty-afikishwa-mahakamani-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE"

Post a Comment

Loading...