Loading...

Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni

Loading...
Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni
link : Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni

soma pia


Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ipo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ‘syllabus’ ya elimu nchini ili wanafunzi waanze kufundishwa maana ya kodi tangu wakiwa wadogo.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa uelewa mdogo katika masuala ya kodi ambao unachangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi hasa wanaoanzisha biashara kuona ulipaji kodi ni mzigo.

 Akizungumza katika mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Rose Mahendeka alisema mchakato huo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzanian Associate kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel and Fernandes Communications, yalilenga kuwakuelimisha jamii kuhusu masuala ya kodi. Aidha, Mahendeka alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutoelewa umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi katika biashara zao.

“Wafanyabiashara wengi hawana uelewa wa kodi ila tupo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ya elimu waanze kupata wakiwa wadogo kabisa kule mashule ili waanze kupata uelewa wakiwa wadogo kabisa kwamba nini maana ya kodi, inahusu nini na jinsi gani kodi inalipwa Tanzania, tunaamini kwa njia hiyo watu wengi wataelewa,” alisema.



Hivyo makala Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni

yaani makala yote Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/elimu-ya-kodi-kuingizwa-kwenye-mitaala.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni"

Post a Comment

Loading...