Loading...
title : Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi
link : Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi
Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi
Na Mwandishi Wetu
Elimu zaidi na kampeni inahitajika kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya Ukimwi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge wakati akizungumza katika wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani iliyoambatana na matembezi ya hisani na mauzo ya tisheti kwa ajili ya kuchangia mfuko wa mapambano dhidi ya Ukimwi.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alisema ipo mikoa takwimu za maambukizi mapya zinapanda huku maeneo mengine hali ikibaki kuwa vile vile.
Aliwataka wananchi kubadili tabia hasa kujitokeza kupima kujua afya zao ili kama wameathirika basi waanze kutumia dawa.
Shekimweri alisema juhudi za makusudi zinatakiwa kuhakikisha mapambano dhidi ya maradhi hayo yanaongezeka .
Alisema mkoa wa Dodoma, mathalani kwa sasa maambukizi mapya yamefikia asilimia 5 yakipanda kwa asilia mbili zaidi ya ilivyokuwa miaka 2011/12.
Lakini alisema maeneo kama ya Zanzibar maambukizi yamepungua na kusema ipo haja ya kutafiti na kueneza majibu ya utafiti kwa umma ili uweze kujihami na maambukizi mapya.
Alisema watu kama Zanzibar inaonekana wamefanya vyema kutokana na kuwa na taratibu njema za kuzuia ‘ngono’ zembe ikiwa na pamoja na matumizi mazuri ya nyumba za kulala wageni.
Pamoja na kuhimiza elimu na utafiti kuzuia maambukizi mapya alizungumzia haja ya kushawishi wadau zaidi kuchangia mfuko wa Ukimwi ambapo kilomita 5 za matembezi ya hisani zimechangia sh 14,500.000 kwa mauzo ya fulana na ahadi mbalimbali.
Alisema ipo haja ya kuandaa mkakati mpya wa kuwezesha kutunisha mfuko huo wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi ambao unahitaji zaidi ya shilingi bilioni tatu. Mkakati huo ni pamoja na kufanya harambee na kutengeneza bidhaa za mauzo kwa ajili ya mfuko.
Aliongeza kuwa mtu binafsi, taasisi au makampuni ambao wangependa kushiriki zoezi hili endelevu la kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi (ATF) wanaweza kutuma michango yao kupitia namba za 0684909090.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri (katikati) akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa (kushoto).
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko akizungumza kuhusu maandalizi pamoja na kuhamasisha uchangiaji wa hiyari unaohusisha mtu binafsi, taasisi mbalimbali za serikali, sekta binafsi na makampuni kupitia 0684909090 wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za serikali, wananchi pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari Dodoma walioshiriki matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa NACOPHA wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi
yaani makala yote Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/elimu-zaidi-inahitajika-mapambano-dhidi.html
0 Response to "Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi"
Post a Comment