Loading...

Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania.

Loading...
Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania.
link : Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania.

soma pia


Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania.

Waziri wa kilimo Nchini Mh Japhet Hasunga anatarajia kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kisera wa Baraza la Kilimo Tanzania unaotarajiwa kufanyika Nov 26 na 27 mwaka huu jijini Dra es salaam wenye lengo kukusanya maoni ya yahusuyo Sera za Kilimo ili kuona namna zinavyoweza kufanyiwa marekebisho. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko imesema mkutano huo wenye kauli mbiu ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania unatarajiwa kuhudhuliwa na wadau wa sekta ya kilimo zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya nchi.

Bi Janeth alitaja mada zitakazowalishwa katika mkutano huo kuwa ni apmoja na mada kuu ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania, Fursa ya Sekta Binafsi Katika Utekelezaji wa ASDP II, Nafasi ya Vijana na Utekelezaji wa ASDP II ikiwa ni pamoja na Kuimarisha Ushirika kwa Faida ya Wazalishaji.

“ Kwetu Baraza la Kilimo Mkutano huu ni muhimu kwa sababu ndiko tunapopata changamoto za kisera zinazowakabili wadau wa kilimo nchini na kwenda kukaa meza moja na serikali na kuzifanyia kazi, ndio maana utaona tumewaalika wadau wote wa kilimo nchini,

“ Na tumegusa wadau wote wanaojihusisha na mboga mboga, maziwa, mifugo kwa ujumla, kilimo , Uvuvi na yeyote anayeguswa na sekta nzima ya kilimo tunaamini kwa kuwaweka pamoja wote hawa tutatoka na maazimio mazuri yatakayolenga kuendelea kuiboresha sekta ya kilimo nchini” alisema Bi Janeth Bitegeko Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Kilimo Tanzania.

Katika mkutano huo na vyombo vya habari ofisini kwake aliongeza kuwa “ Mambo yote yatakayojadiliwa katika mkutano huu ndio kipaumbele chetu kwa mwaka ujao 2019, kwasababu tumekuwa tukiyafanyia kazi na kumekuwa na matokeo chanya kwasababu sisi tumekuwa tukifanya kazi na serikali kwa karibu zaidi ndio maana unaona masuala mengi yaliyokuwa changamoto kwa wakulima kama vile tozo serikali imekwisha kuyafanyia kazi”.


Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku mbili cha Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo, kulia kwake ni Makamo Mwenyekiti Bi Jacqueline Mkindi . 
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akiwa katika moja ya vikao vya Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania. 



Hivyo makala Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania.

yaani makala yote Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/hasunga-kufungua-mkutano-wa-baraza-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania."

Post a Comment

Loading...